Shaker (Lil Shaker)

Mwanamuziki wa Ghana


Elikplim Yao Atiemo (alizaliwa Accra, Ghana), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Shaker (Lil Shaker), ni msanii wa kurekodi wa Ghana, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji na mwigizaji. Kwa sasa amesajiliwa kwa kampuni kubwa ya rekodi na media media ya Ghana, BBnZ Live ambayo pia ina wasanii kama EL. Anazo nyimbo kama vile ‘I No Dey See U Saf’ na ‘Madakraa’ na pia ametayarisha Sarkodie ‘Talk Of Gh’ na ‘Lies’[1].

Shaker
Lil Shaker
Lil Shaker
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Elikplim Yao Atiemo
Pia anajulikana kama Lil Shaker
Asili yake Accra, Ghana
Miaka ya kazi 2004 - hadi leo
Tovuti www.bbnz-live.com

Maisha ya awali

hariri

Elikplim Yao Atiemo alizaliwa Accra , mji mkuu wa Ghana na wazazi Waghana wenye asili ya Mkoa wa Volta. Alianza kazi yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 15. Kwa sasa amesajiliwa kwa lebo kubwa zaidi ya rekodi ya Ghana na kampuni ya media, BBnZ Live[2].

Ushirikiano na Ushawishi

hariri

Shaker, ameshirikiana na wasanii kama vile Sarkodie, EL, Raquel, Wanlov the Kubolor, Edem, Gemini na wengine wengi.

Rekodi

hariri

Oktoba 2015, Shaker alijiunga na Ko-Jo Cue, Cwesi Oteng na E.L katika BBNZ Live[3][4]

Marejeo

hariri
  1. https://www.ghbase.com/10-ghanaian-musicians-who-are-amazing-beatmakers/
  2. http://www.bbnz-live.com/projects/shaker.html
  3. https://ameyawdebrah.com/lil-shaker-joins-e-l-cwesi-oteng-bbnz-live/
  4. https://www.nydjlive.com/guess-which-actress-bbnz-live-artist-lil-shaker-has-a-crush-on/
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shaker (Lil Shaker) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.