The Star (mara nyingi hujulikana kama Sheffield Star) ni gazeti la kila siku linalochapishwa Sheffield, Uingereza kutoka Jumatatu hadi Jumamosi kwa wiki. Hapo mwanzoni, mtindo wake wa uchapishaji ulikuwa mpana lakini ukabadilishwa kuwa mdogo katika mwaka wa 1989. Magazeti ya The Star,The Sheffield Telegraph na The Green Un yanachapishwa na Kampuni ya Magazeti ya Sheffield (inayomilikiwa na Johnson Press) ambayo ina makao yake katika barabara ya York Street katikati mwa jiji la Sheffield.

The Star
Jina la gazeti The Star au Sheffield Star
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1887
Nchi Uingereza
Mhariri Alan Powell
Mmiliki Johnston Press
Mchapishaji Kampuni ya Magazeti ya Sheffield
Makao Makuu ya kampuni Sheffield
Machapisho husika Doncaster Star
Sheffield Telegraph
Tovuti http://www.thestar.co.uk/
Ukiangalia Barabara ya High Street karibu na makutano ya High Street na Fargate, jengo la Star & Telegraph Building liko kwenye upande wa kushoto

The Star linauzwa katika maeneo kama Yorkshire Kusini, Derbyshire Kaskazini na Nottinghamshire Kaskazini. Huweza kufikia wasomaji wake kwa kupitia matoleo makuu na matoleo ya wilaya kama Doncaster, Rotherham na Barnsley. Jumla ya wastani ya wasomaji wa kila toleo la The Star ni 159,690.

Gazeti hili la The Star lilianza kama Sheffield Evening Telegraph. Toleo la kwanza la gazeti hili lilichapishwa mnamo 7 Juni 1887. Baada ya muda mfupi, lilinunua gazeti shindani ,Sheffield Evening Star. Tangu Juni 1888 mpaka Desemba 1897 gazeti hili lilijulikana kama Evening Telegraph and Star and Sheffield Daily Times kisha,kutoka mwaka wa 1898 mpaka Oktoba 1937 likajulikana kama Yorkshire Telegraph and Star. Tangu mwaka wa 1931, lilinunua gazeti la Sheffield Mail ambalo lilikuwa gazeti shindani lake tangu mwaka wa 1920. Tangu mwaka wa 1937 mpaka mwezi wa Novemba 1938, gazeti hilo likawa Telegraph & Star. Hatimaye likachukua jina lake la The Star mnamo 14 Novemba 1938,hadi sasa .bad linaitwa jina hilo.

Joshnston Press ikaanza kuchapisha The Star katika kiwanda chao kipya cha uchapishaji cha thamani ya £ milioni 60 katika eneo la Dinnington karibu na Sheffield mnamo Septemba 2006. Kiwanda hiki kinajumuisha kifaa cha uchapishaji wa 'upana wa mara tatu' cha kwanza nchini Uingereza. Kitakapomalizika kamili, kiwanda hiki hakitachapisha magazeti ya Johnston Press kama Sheffield Telegraph, the Scarborough Evening News, Wakefield Express, the Derbyshire Times na Chesterfield Advertiser tu bali kuchapisha majarida mengine ya nje kama The Sun la News International.

Mwezi wa Machi 2006, mwandishi wa michezo katika gazeti la Sheffield Star , Martin Smith, alishinda tuzo ya taifa kutoka British Sports Journalism Awards, tamasha la kutuza waandishi la umri wa miaka zaidi ya 30. Alipewa tuzo ya mwandishi wa habari ya spoti wa eneo lake wa mwaka haswa Regional Sports Writer of The Year. Hii ilikuwa mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo katika miaka mitatu. Alituzwa na muungano wa Sports Journalists' Association of Great Britain.

Mhariri wa sasa wa gazeti la Sheffield Star ni Alan Powell.

Tanbihi

hariri
  1. Joint Industry Committee for Regional Press Research (JICREG) Ilihifadhiwa 13 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. 1 Januari 2007
  2. Newspapers Catalogue of the British Library Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
  3. Journalism jobs and news from Holdthefrontpage.co.uk Ilihifadhiwa 2 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
  4. Journalism jobs and news from Holdthefrontpage.co.uk Ilihifadhiwa 5 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.

Marejeo

hariri
  • Bob Horton, Living in Sheffield: 1000 years of change

Viungo vya nje

hariri