Sherine Tadros ni mwandishi habari Mwarabu-Muingereza anayeripotia kutoka bara la Mashariki ya Kati. Yeye ni mwanahabari wa Al Jazeera ya Kiingereza, moja ya stesheni inayoongoza duniani iliyo na makao makuu jijini Doha, Qatar. [1][2][3]

Sherine Tadros

Wakati wa vita vya Israeli na Gaza mwaka wa 2008-2009, Sherine na mwandishi mwenziwe wa Al Jazeera, Ayman Mohyeldin, walikuwa waandishi pekee wa kutoka stesheni yenye kutumia lugha ya Kiingereza kote duniani wliokuwa wakiripotia kutoka ndani ya Gaza. Vyombo vya kigeni vya habari vimekuwa vikizuiliwa kuingia Gaza kwa kupitia Misri au Israeli. Hata hivyo, Ayman na Sherine tayari walikuwa ndani ya Gaza wakati vita vilianza.[4][5][6][7]

Elimu na wasifu

hariri

Sherine ana shahada mbili katika siasa za Mashariki ya kati na alifundisha som la siasa kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza katika SOAS, Chuo Kikuu cha London.

Alianza kazi yake ya uandishi kama mtayarishaji mkuu wa Al Arabiya jijini London, akifanya kazi kote Ulaya kwa mtandao huu wa Dubai. Yeye aliongoza wanahabari wenziwe katika uchaguzi wa Uingereza mnamo mwaka 2005 na kuripotia kuhusu mabomu ya London mwaka huo huo.

Mwaka wa 2005, alijiunga na Al Jazeera, jijini London na mwaka mmoja baadaye alihamia Doha kama mwandishi / mtayarishaji, akitangaza taarifa kutoka kote duniani: kutoka Marekani hadi nchi za Arabuni. Ripoti zake maarufu ni kama ya Hamas kupata umiliki wa Gaza, pilkapilka za kushindania urais wa Marekani na Beirut kukamatwa na Hezbollah mnamo Mei 2007.[8]


Marejeo

hariri
  1. [1] ^ Al-Jazeera says its English-language news channel will launch Nov. 15
  2. A new channel fika
  3. BBC World imeshuka kwa Israel satellite TV
  4. [24] ^ Al-Jazeera becomes the face of the frontline Financial Times
  5. Israeli banar väg zaidi ndani ya Gaza
  6. [23] ^ Al Jazeera English Beats Israeli's Ban on Reporters in Gaza with Exclusive Coverage The HUFFINGTON POST
  7. Gaza, African chanjo na tonight's RTS tuzo - breakfast table chat na Al Jazeera
  8. Al Jazeera Kiingereza - Kuhusu sisi - Field kontaktpersoner

Viungo vya nje

hariri