Kanieneo angahewa

(Elekezwa kutoka Shinikizo la hewa)

Kanieneo angahewa (pia: shinikizo la hewa) ni nguvu inayosukuma dhidi ya uso wa dunia na kila kitu au kiumbe kutokana uzito wa hewa iliyoko katika angahewa ya dunia juu yake.

Mstari buluu unaonyesha jinsi gani kanieneo angahewa inategemeana na kimo juu ya uwiano wa bahari: kadri mahali iko juu mlimani kanieneo inapungua.

Uzito wa hewa

hariri

Juu ya kila mahali duniani kuna uzito wa nguzo ya hewa yenye urefu wa takriban kilomita 500 hadi mwisho wa angahewa. Uzito huu ni mkubwa kwenye pwani la bahari ambako ganda la hewa juu ya mahali ni nene. Lakini uzito huu na hivyo kanieneo ni mdogo zaidi juu ya milima mirefu ambako umbali hadi mwisho wa angahewa ni mdogo zaidi. Kwa wastani uzito wa nguzo ya hewa juu ya mita ya mraba moja kwenye uwiano wa bahari ni tani 10 lakini kipimo hiki kinaonyesha mabadiliko kutokana na mabadiliko ya kanieneo angahewa mahali hapa.

Vipimo vya kanieneo angahewa

hariri

Kipimo cha kanieneo angahewa ni hektopaskali na kanieneo kwenye uwiano wa bahari inalingana takriban na hektopaskali 100. Lakini kuna pia vipimi vingine vilivyo kawaida katika nchi nyingine , kati ya hai ni bar.

Chombo cha kuipimia kinaitwa barometa.[1]

 
Chupa kilichovunjwa na kanieneo angahewa kwenye uwiano wa bahari; ilijaa hewa na kufungwa katika kimo cha mita 4,500 juu ya UB ambako kanieneo ni ndogo.

Kanieneo angahewa na viumbehai

hariri

Viumbe vyote hutegemea kanieneo jinsi ilivyo kawaida kwao. Kimsingi mwili wa binadamu inaweza kuathiriwa kama chupa cha plastiki katika picha hapo upande wa kulia. Tunavumilia kanieneo ya kawaida ya angahewa kwa sababu kiowevu vya seli zetu na damu kina shinikizo ya kulingana. Kama tunapanda sana juu tuko hatarini ya kulipuka kwa sababu shindikizo ya angahewa inapungua kwa hiyo shindikizo ya ndani ya miili yetu inaweza kupasua ngozi yetu. Lakini hata kabla kufika juu vile kunatokea matatizo kwa sababu uwezo wa damu kushika na kubeba oksijeni inapungua pia na hjii ni sababu ya kwamba ndege kubwa zinazotembea katika kimo cha mita 11.000 au zaidi huwa na chumba ambako kanieneo angahewani inaongezwa kwa njia ya mitambo. Ndege zinazofikia juu zaidi au marubani wa roketi ni lazima watu wawe na nguo zinazotunza shinikizo ndani.

Kinyume chake kuna viumbe wanaoishi chini ya bahari katika kina kubwa penye shinikizo ya juu katika maji na wanyama hao wakifikishwa kwenye uso wa bahari sharti wanakufa kwa sbabau ya tofauti kubwa ya kanieneo.

Marejeo

hariri
  1. "atmospheric pressure -- Britannica Online Encyclopedia". britannica.com. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2010.

Viungo vya Nje

hariri