Shinto au Ushinto ni dini ya jadi nchini Japani. Hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa dini rasmi ya serikali na ya Kaisari wa Japani.

Geti la torii kwenye hekalu la Kishinto

Imani ya Shinto ni katika miungu au pepo wengi wanaoitwa "kami". Wengine wao ni kama miungu, wengine ni roho za miti, mito au milima, wengine tena ni mizimu. Kati ya kami muhimu zaidi kuna amaterasu (jua), dunia, mbingu.

Kuna makuhani wanaotunza hekalu ambako sadaka hutolewa kwa kami hizi. Wajapani wengi hushiriki katika ibada za kami, wakikumbuka mababu na marehemu wengine, hata wakifuata dini nyingine kama Ubuddha au Ukristo.

Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shinto kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.