Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Shira (nyota)

Shira ni kimiminika kizito ambacho kimsingi ni mmumunyo wa maji na sukari. Inapatikana kwa kuchemsha maji na sukari au maji ya matunda (yenye sukari ndani yake) na hivyo kupunguza kiwango cha maji ambayo yanavukizwa ilhali sukari inabaki. Inafanana na asali.

Kiwango kikubwa cha sukari kinawezesha kutunzwa kwa shira hata bila friji kama chombo chake kimefungwa vizuri.

Shira hutumiwa kwa kutengeneza vinywaji, katika upishi wa vyakula, kuoka kwa keki na mikate halafu pia kama dawa.