Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (Kiingereza: Tanzania Petroleum Development Corporation TPDC) ni kampuni ya mafuta ghafi (petroli) ya kitaifa ya Tanzania. Inamiliki leseni zote za maendeleo ya vyanzo vya mafuta na gesi nchini. Kampuni ilianzishwa kupitia Tangazo la Serikali Na.140 la tarehe 30 Mei 1969 chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Na.17 ya mwaka 1969. Shirika lilianza kufanya kazi mnamo 1973. Ni shirika la serikali inayomilikiwa kikamilifu na hisa zake zote zikiwa na Msajili wa Hazina. [1]
Mwaka 2015 Bunge la Tanzania lilipitisha sheria zinazohusu mafuta na kazi ya kampuni hiyo: Sheria ya Mafuta ya 2015, Sheria ya Sekta ya Uziduaji Tanzania (Uwazi na Uwajibikaji) ya 2015, na Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya 2015. [2]
Makadirio yanaweka akiba ya gesi nchini Tanzania kwa zaidi ya futi za ujazo trilioni 50. Serikali inadhani idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu wakati visima vya ziada vya uchunguzi vinapochimbwa, na kuvifanya kuwa chanzo kikubwa cha mapato." [3]
Kuna kmapuni tanzu mbili zilizopo chini ya TPDC ambazo ni Gas Supply Company Limited (GASCO) na TANOIL Investments Limited.
Marejeo
hariri- ↑ Sam Moyo; Michael Sill; na wenz. (1 Aprili 1999). Energy policy and planning in Southern Africa. SARIPS of SAPES Trust, Regional Office. ISBN 978-1-77905-096-0.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "EY Global Tax Alert: Tanzania enacts legislation impacting the oil and gas industry" (PDF). Ernst & Young. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-03-29. Iliwekwa mnamo 7 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tanzania's troubles over gas revenue Sharing the spoils". The Economist. 2014-09-09. Iliwekwa mnamo 7 Januari 2016.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)