Shirika la Watoto wa Nakuru

Shirika la Watoto wa Nakuru ni shirika lisilo la faida ambalo linajitahidi kupunguza umaskini na kuboresha elimu kwa watoto huko Nakuru, Kenya[1]. Tangu mwaka 2009, shirika hili limesaidia zaidi ya watoto 2000 kupata elimu bora. [2]Kutokana na kazi ambayo Shirika la Watoto wa Nakuru linafanya, kuna watoto 182 wanaosoma katika shule za sekondari au vyuo vya mafunzo vya ufundi stadi. Pia, watoto wa shule wenye uhitaji wamepatiwa milo zaidi ya 391,655 bure. Zaidi ya madarasa ishrini, vyoo, na ofisi zimejengwa. Familia 368 zilisaidiwa wakati wa UVIKO-19, na watoto 45 wanasoma katika kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum ya kielimu.

Misheni

hariri

Shirika la Watoto wa Nakuru linaamini elimu ni muhimu ili kumaliza mateso ya mtoto na umaskini mkali. Shirika huchukua mtazamo kamili kwa kila mtoto kwa kutoa msaada katika kila ngazi ya elimu ili kuwasaidia watoto kuingia shuleni, kufikia matokeo bora ya kujifunza, na kufikia ndoto zao wenyewe.[3]Kulingana na UNICEF, kila mtoto anastahili elimu ya hali ya juu lakini nchini Kenya, watoto hawapati haki hii ya kimsingi. Baadhi ya shule za msingi hazina vifaa vinavyohitajika. Madarasa yana wanafunzi wengi sana kwa wanafunzi kujifunza kwa ufanisi. Pia, walimu wana kazi nyingi. Mara nyingi watoto maskini watakuja shuleni wakiwa na njaa sana. Watoto wengi hawaendi shule kwa sababu lazima wafanye kazi.

Ili kutimiza misheni hii, Shirika la Watoto wa Nakuru linafanya kazi na shule za watoto na shule za msingi kujenga nyenzo muhimu, kutoa chakula cha mchana shuleni bure, na kuboresha kiwango cha elimu. Hii husaidia watoto kupata matokeo bora zaidi ya mitihani. Pia, wanalipa ada kwa familia ambazo haziwezi kumudu. Wanatoa mwongozo na ushauri ili kuwasaidia kushinda changamoto mbalimbali.

"Watoto wetu watakuwa viongozi wa kesho wa Kenya, kupigania mustakabali ambao ni sawa kwa wote." -Shirika la Watoto wa Nakuru

Miradi ya baadaye

hariri

Shirika la Watoto wa Nakuru lilinunua ekari mbili za ardhi ndani ya jamii yenye umaskini mkubwa. Ndoto yao ni kujenga ardhi hii kuwa kituo cha kuhudumia jamii. Hii itajumuisha kuleta milo ya shule bure kwa shule za chekechea na shule za msingi, kujenga nyumba za dharura, kujenga ofisi ya mfanyakazi wa kijamii kusaidia vijana ambao hawajiwezi, na kukuza chakula chao wenyewe. Mahali hapa patakuwa kitovu ambacho kinaweza kusaidia watoto ambao hawajiwezi kufaulu ndani ya mfumo wa elimu wa serikali.

Kufikia mwaka wa 2025, Shirika la Watoto wa Nakuru linataka kutoa milo 3,000 ya shule bure kwa wiki kutoka jikoni yao ya jamii, wakikuza mazao yao wenyewe ili kujiendeleza.

Marejeo

hariri
  1. "Nakuru Children's Project". Global Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-12.
  2. "Nakuru Children's Project". Nakuru Children's Project (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-12-12.
  3. "The Convention on the Rights of the Child: The children's version". www.unicef.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-09.