Shirley Abbott (mwanakandanda)
Shirley Wray Abbott (10 Februari 1889 - 26 Septemba 1947) alikuwa mwanakandanda wa kulipwa raia wa Uingereza na nahodha wa klabu kama Chesterfield pia Portsmouth katika ligi kuu Uingereza.[1]
Akiwa kiungo mkabaji alicheza katika klabu mbili tofauti zilizokuwa ligi kuu ikiwemo Queens Park Rangers na Derby County; baada ya kustaafu kucheza kandanda aligeukia kwenye ukufunzi wa kandanda katika klabu ya Chesterfield F.C. mwaka 1928 hadi mwaka 1939.[2][3]
Maisha binafsi
haririKipindi cha Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alihudumu kwenye kikosi cha jeshi London na baada ya vita kuisha alimaliza na cheo cha sajenti.[4] Vita ya pili ya dunia alihudumu kama mpakia na mpakua mizigo katika mji Portsmouth, mwaka 1947 alifariki kwa saratani.
Marejeo
hariri- ↑ "Shirley Abbott | Chesterfield | Club | Past Players | Past Players". web.archive.org. 2008-05-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-13. Iliwekwa mnamo 2024-08-09.
- ↑ https://web.archive.org/web/20080513151653/http://www.chesterfield-fc.premiumtv.co.uk/page/PastPlayersDetail/0,,10435~73267,00.html
- ↑ "Abbott Shirley Image 3 Portsmouth 1920". Vintage Footballers (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-08-09.
- ↑ "Shirley Wray Abbott | Service Record". Football and the First World War (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-08-09.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shirley Abbott (mwanakandanda) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |