Shule ya Maru-a-Pula

Shule ya Maru-a-Pula ni shule ya sekondari ya kutwa na bweni, ya jinsia za aina zote ya kiume na ya kike na ni shule ya kujitegemea huko Gaborone, Botswana. Ilianzishwa mwaka 1972.

Shule hiyo inawajengea wanafunzi uwezo wa mitihani ya Cheti cha Kimataifa cha Elimu cha Cambridge(IGCSE), Kiwango cha Juu cha Msingi (AS) na Ngazi ya elimu ya juu ya sekondari. Inashika nafasi ya juu kati ya shule za sekondari nchini Botswana na inatoa maandalizi makini kwa mitihani ya Cambridge IGCSE, AS na Ngazi ya elimu ya juu ya sekondari. Wanafunzi wa Maru-a-Pula wamepokea tuzo za Juu Duniani "Top in the World" za Cambridge kwa mafanikio yao makubwa katika mitihani ya IGCSE na ya Ngazi ya elimu ya juu ya sekondari na wahitimu 64 kwa sasa wanafanya masomo yao katika vyuo vikuu vilivyoorodheshwa katika nafasi ya 100 bora duniani.[1]

Marejeo

hariri
  1. "Top 10 Secondary Schools in Botswana". Serve Africa (kwa American English). 2020-09-04. Iliwekwa mnamo 2024-07-16.