Shule ya Upili ya Alliance

Shule ya Upili ya Alliance ilianzishwa 1 Machi 1926 na Muungano wa Makanisa ya Kiprotestanti, Kanisa la Scotland Mission (inayojulikana kama Kanisa la Afrika Mashariki au PCEA en:Presbyterian Church of East Africa), Kanisa la Jimbo ya Kenya (CPK en:Church of the Province of Kenya), African Inland Church (AIC), na Kanisa la Methodist(en:Methodist Church). Alliance ilikuwa shule ya kwanza nchini kutoa mafunzo ya sekondari kwa wanafunzi wa asili ya Kiafrika humu nchini Kenya.

Shule ya alliance

Shule hii iko Kikuyu, Kenya, takriban kilomita 22 (maili 12) kutoka Nairobi. Alliance ni jirani na shule ya wasichana ya Alliance. Shule hizi mbili zimekuwa na uhusiano kama wa ndugu na dada tangu jadi. Shule ya Upili ya Alliance inasifika sana kwa historia yake tajiri na ubora wa elimu. Alliance imekuwa ikiongoza katika uwanja wa elimu kwa zaida ya miongo nane. Imeorodheshwa katika shule kumi bora tangu uanzilishi wake. Iliorodheshwa kama shule bora nchini katika mwaka wa 2005 katika matokeo ya mtihani ya Kenya Certificate of Secondary Education [1] Archived 10 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.. Mwaka 2006 iliorodheshwa kama shule ya tatu nchini [2][dead link].

Shule hii inajivunia wanafunzi wake ambao wanafunzwa kuwa hudimia wenzao bila kuchoka. Wanafunzi wenye vipaji mbalimbali na tamaduni mbalimbali wanakubaliwa kuendeleza ubora wao katika nyanja zote za shughuli za shule. Alliance inajivunia kuwafunza wengi ambao wamefaulu katika Nyanja zote nchini. Chama cha wanafunzi wa kitambo wa Alliance imezidi kuboreka kila mwaka. Mwalimu Mkuu wa sasa ni bwana David Kariuki aliyeshikilia uogozi baada ya Mkuu wa zamani,Christopher Situma Khaemba kwenda kuongoaza shule ya Africa Leadership Academy.

Mtaala hariri

Alliance High School hufuata mfumo wa 8-4-4 na huwatayarisha wanafunzi wake kufanya mtihani wa KCSE. Alliance hutoa mafunzo katika masomo zaidi ya ishirini na moja. Baadhi ya masomo yanayotolewa na Alliance yameorodheshwa hapa chini: Hisabati, Kemia, Kiingereza, Jiografia, Historia, Dini ya Kikristo , Kiswahili, Biolojia, Somo la tarakilishi, Kilimo, Fizikia, umekanika, Uchoraji, Somo la Umeme, Kifaransa, Muzuki, Kijerumani na biashara. Mtaala huwapa wanafunzi wa huwapa wanafunzi fursa ya kuchagua masomo ambayo yatawafaidi katika kazi zao za baadae. Alliance huwawezesha wanafunzi wake kuingia katika mipango inayo heshimika katika vyuo kikuu. Wanafunzi waliohitimu kutoka Alliance wanaendeleza masomo yao katika vyuo vikuu mbalimbali kote duniani. Angalau kila mwaka wanafunzi watano husajiliwa katika vyuo vinavyo heshimaka huko marekani(Ivy league).

Mtaala wa ziada hariri

Katika kutekeleza azma yake ya kuwalea wanafunzi wasio tu wapevu kiakili, bali pia kimwili na kitabia, shule hii inamtaala wa ziada unaowasaidia wanafunzi wake kuboresha vipaji vyao, kukuza ujuzi wa uongozi na kupanua fikira zao. Mtaala huu waziada inajumuisha drama, kwaya, machapisho kama vile gazeti ya shule; uongozi wa shule kupitia ukaranja(ambayo inasifika kote nchini); huduma kwa jamii, Kufunza watoto wadogo na kutembelea wagonjwa na wazee, maskauti, chama cha mjadala, chama cha mazingira, chama cha biashara, chama cha ukulima, chama cha waandishi(linayo chapisha gazeti shule maarufu kama “Bush fire”), chama cha Sayansi, chama cha utarakilishi. Pia kuna fursa ya kutembea nchi mbalimbali kupitia mpango na chuo cha Brooks kule Marekani na chuo cha Sir John Leman kule Uingereza. Wengine hutembelea Ufaransa ilikujifunza kuishi na watu waliona mila tofauti. Mnamo mwaka wa 2004, kwaya ilinyakua tuzo sita katika mashindano ya kitaifa ya muziki. Kwaya ilishinda udhamini wa ziara ya siku 28 kule Marekani katika mwaka wa 2002. Udhamini huu ulitolewa na shirika la Outreach Foundation.

Michezo hariri

Wanafunzi hupata fursa ya kujiunga na timu mbali mbali za michezo. Wanafunzi wanafunzwa umuhimu wa michezo na ushirikiano katika timu.Michezo hizi zinajumuisha mchezo wa kikapu, raga, kabumbu, riadha, mchezo wa magogo, voliboli, kuogelea na tenisi. Alliance hushindana dhidi ya shule zingine katika michezo hizi zote. Timu hizi zimeshinda medali kadha wa kadha. Timu ya magongo ilipigiwa kura na ikaibuka timu ya tatu bora nchini mnamo mwaka wa 2002. Mwaka huo huo wa 2002 timu ya magongo ilishinda mashindano ya kitaifa. Timu ya raga nayo ilinayakua ushindi katika mashindano ya Prescot mnamo mwaka wa 2003.

Watu maarufu waliosomea Alliance hariri

  1. Marehemu George Anyona- Mbunge wa zamani, Kenya;
  2. Kiraitu Murungi - Waziri wa Nishati, Kenya;
  3. W. Makau Mutua – Buffalo Law School, State University of New York, Mwenyekiti, Kenya, Tume ya Haki za Binadamu;
  4. Mwiraria David - Mbunge wa zamani, Kenya;
  5. Marehemu Paul Ngei - Aliyekuwa Waziri na mpiganaji wa Maumau;
  6. Charles Njonjo - Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya;
  7. Anyang’ nyongo - Mjumbe wa Bunge, Kenya;
  8. Ngugi wa Thiong'o - Mwandishi na mwalimu;
  9. Amos Wako - Mwanasheria Mkuu, Kenya;
  10. Marehemu Ngala Mwendwa - Aliyekuwa Mbunge na Waziri, Kenya;
  11. Kenneth Matiba - Aliyekuwa mgombea urais, Mbunge na Waziri, Kenya;
  12. Margaret Kenyatta – Mwanamke wa kwanza kuwa Meya wa Nairobi;
  13. Joseph Ole Wagur - Katibu Mkuu, Tume ya Kriegler;

Wimbo wa shule hariri

Bwana, tukiwaobea wanadamu wote, kutoka kila sehemu, tusikize eeh bwana na usaidie shule yetu, shule tanayoipenda sana.(×3)]].

Sala ya Shule hariri

Iweke mikononi mwako, Ee Bwana, shule hii, ilikazi yake iwekamilifu na maisha yake yenye furaha, iwatoe wanaume walioimarika kimwili, kiakili na kitabia na kwa jina lako na nguvu zako wawatumikie wenzao kikamilifu. Amina.

Ujumbe wa ziada Shule hii inajulikana na jina la kiutani “BUSH”. Jina hili lilitokana na misitu inayo zunguka Alliance kutoka kila upande. Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Alliance huita shule hii “Across”, kwa kuwa shule hizi mbili zimetenganishwa na bonde.

Viunganishi vya nje hariri

  1. Alliance High School [3]
  2. Alliance Girls High School [4] Archived 30 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
  3. Alliance High School Alumni Foundation [5] Archived 10 Februari 2005 at the Wayback Machine.
  4. KCSE: Alliance Boys yang'aa makala Eaststandard.net 1 Machi 2006 [6] Archived 10 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.

Tazama pia hariri

  1. Rev Dk Yohana Arthur marejeleo ya ziada
  2. J. Stephen Smith, Historia ya Alliance High School (Nairobi: Heinemann, 1973)
  3. Taasisi za elimu mwaka wa 1926
  4. Shule nchini Kenya
  5. Elimu mjini Nairobi
  6. Elimu katika Mkoa wa Kati (Kenya)