Siagi ya karanga ni chakula chenye umbo la malai ambayo inatengenezwa kwa kutumia karanga zilizokaangwa.

Siagi ya karanga.

Karanga zinasafishwa baada ya kukaangwa halafu zinasagwa. Wakati wa kusaga mafuta yaliyopo ndani yake yanatoka; kama hamna ya kutosha, mafuta huongezwa na yote inakorogwa hadi kufikia hali ya malai laini. Tokeo lake linafanana kiasi na siagi na pia inaweza kuliwa kama siagi, mfano: kwa kupakwa juu ya mkate. Hivyo jina "siagi ya karanga" limetokea ingawa malai hii haina uhusiano wa kweli na siagi inayotengenezwa kutokana na maziwa ya wanyama ilhali "siagi ya karanga" inatokana na mimea pekee.

Siagi ya karanga inaweza kukaa muda mrefu bila ya kuharibika au kuchacha pasipo kuongezewa kemikali yoyote ndani yake. Viungo vinavyohusika katika kutengeneza siagi hii ni karanga, chumvi, mafuta ya kupikia na sukari.

Inaongeza protini mwilini na huleta ladha tamu katika chakula.

Hivyo siagi hii hutumika kwenye mapishi: unaweza kuiweka katika nyama,kande, mboga za majani na hata kupaka juu ya mkate.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siagi ya karanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.