Siku ya Matendo Mema

Siku ya Matendo Mema ni siku ya kimataifa ya kujitolea iliyoanza mwaka 2007. Siku hiyo hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Machi au Aprili.

Alama ya Siku ya Matendo Mema duniani

Lengo ni kuunganisha watu wengi duniani kwa ajili ya kufanya matendo mema kwa wengine na kwa ajili ya dunia.

Siku hiyo ya huduma za kijamii ilizinduliwa mara ya kwanza nchini Israel na mfanyabiashara mwanamke mhisaniShari Arison, kupitia Ruach Tova, ambayo ni asasi isiyo ya kifaida ambayo inaunganishwa watu wanaotaka kijitolea pamoja na taasisi nyingine. Kuzungumzia kuhusu siku hii, Shari Arison amesema: 'Ninaamini kwamba kama watu wote watafikiri mambo mema, kuzungumza mema na kutenda mema, mzunguko wa kutenda mema utaongezeka duniani, siku ya matendo mema imekuwa siku yenye muhamko mkubwa wa utoaji wa matumaini, na mwaka huu watu binafsi, watoto wa shule, wanajeshi na wafanyakazi kutoka katika shughuli nyingi mbalimbali wanaungana kwa ajili ya siku ya matendo mema ya mwaka, kwa ajili ya kufanya matendo mema kwa wengine kama kumbukizi' [1].

Historia

hariri

Katika Israeli

hariri

Siku ya Matendo (kwa Kiyahudi: יום המעשים הטובים) ilianza mwaka 2007. Kwa makadirio ya watu wapatao 7,000 walishiriki nchini Israel katika mwaka huo.

Hadi mwaka 2016 walifikia watu 1,500,000. Kampuni mbalimbali zikishiriki pamoja na asasi zisizo za kifaida nchi nzima kwa kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii, kama vile kupaka rangi majengo, kupanda bustani za kijamii pamoja na mambo mbalimbali yanayohitajika katika jamii, miji kama Tel Aviv na Yerusalemu ziliandaa matamasha maalumu ya wazi.

Uungwaji mkono na Dunia

hariri

Kufikia mwaka 2011 dunia nzima ilianza kushiriki ikijumuisha Marekani, Ukraine na Poland. Mwaka 2011, kampuni za kimataifa Shikun & Binui na Bank Hapoalim zilikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza ya kimataifa kushiriki katika siku ya matendo mema nje ya Israeli, siku ya matendo mema imekuwa ikisherehekewa katika miji mikubwa kama Roma, São Paulo, Kaohsiung City, na New York City kwa kuandaa matamasha maalumu. Katika siku hiyo katika eneo la Herald Square, New York City, msanii na mwigizaji Adrian Grenier aliunga mkono kwa kuzungumza katika siku ya tamasha

ni muhimu kuwa na siku ambayo itawafanya watu kuyafikiria zaidi kufanya mammbo mazuri .[2]

Mwaka 2012, mpango huu uliungwa mkono na MTV na kufanya kampeni ya wiki sita katika runinga yake ya mtandaoni, na ujumbe kuwafikia zaidi ya watu milioni 24 duniani.

Papa Fransisko akishiriki siku ya matendo mema 2015 mjini Roma alisema:

nina tuma ujumbe wangu kwa wote wanaojitolea kuwa wanapaswa kuungana na kuonyesha utu wa kufanya mambo mazuri ili kuitengeneza jamii iliyo bora.[3]

Mwaka 2016 siku ya matendo mema nchini Brazil walifikia watu 10,000 nchi nzima, na miji 40 ya Brazili ikijumuisha miji mikubwa kama Rio de Janeiro, Brasília, na São Paulo.

Katika Amerika ya Kilatini, tukio kubwa lilifanyika Panama, Costa Rica, Brazil, Peru, na nchi nyingine 16.

Huko Taiwan, siku ya matendo mema iliungana na TAVE (Taiwan Association for Volunteer Effort) kufanya shughuli kubwa katika miji mikubwa ya Kaohsiung City, Taiwan 2016. Makamo wa Raisi, Chen Chien-jen, na Kaohsiung’s Mayor, Chen Chu, walikuwa miongoni wa wageni wa heshima waloshiriki siku hii.[4] Taoyuan City ulisherehekea siku hii , na kuandaliwa na Taoyuan City Volunteer Service Association na asasi nyingine shiriki.[5]

Mwaka wa 2020 ni mwaka wa 14 wa siku ya matendo mema, kwa makadirio zaidi ya nchi 93 zitashiriki na jumla watu 2,500,000 watajitolea duniani, siku hii husherehekewa na nchi kama Kenya, Tanzania, Ureno, Italia na nchi nyingine.

Siku ya matendo mema na Ruach Tova ni sehemu ya Ted Arison Family Foundation, na mhisani wa Arison Group.

Tarehe

hariri
Mwaka Tarehe ya Israeli Tarehe ya kimataifa
2007 Mei 8 N/A
2008 Machi 24 N/A
2009 Machi 25 N/A
2010 Machi 16 N/A
2011 Aprili 5 Aprili 5
2012 Machi 20 Machi 25
2013 Machi 3 Machi 10
2014 Machi 11 Machi 9
2015 Machi 24 Machi 15
2016 Machi 15 Aprili 10
2017 Machi 28 Aprili 2
2018 Machi 13 Aprili 15
2019 Aprili 2 Aprili 7
2020 Machi 24 Machi 29
2021 Machi 16 Aprili 11
2022 Machi 29 Aprili 3
2023 Machi 21 Aprili 16
2024 Aprili 9 Aprili 14
2025 Aprili 1 Aprili 6


SIku ya Matendo Mema imepokea tuzo ya George W. Romney Affiliate Excellence Award ya 2016.[6]

Tazama Pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. 900,000 people take part in Good Deeds Day (Israel21c)
  2. Adrian Grenier speaks in the 2016 Good Deeds Day Event at Herald Square, New York City (Youtube)
  3. "Pope honors Good Deeds Day (Shari Arison)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-11. Iliwekwa mnamo 2020-03-08.
  4. (TaiwanHot, in Chinese)
  5. "(Now News, in Chinese)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-03. Iliwekwa mnamo 2020-03-08.
  6. Good Deeds Day won the 2016 George W. Romney Affiliate Excellence Award (PR Newswire)

Viungo vya Nje

hariri