Siku ya Tabia Nchi 2020

Maadhimisho ya siku ya tabia nchi ni mpango mkakati na maandamano wa dunia nzima uliofanyika Septemba 25 mwaka 2020, ulioandaliwa na Fridays For Future na mashirika mengine kama Youth for Climate na 350.org. maandamano ni sehemu ya shughuli za Fridays For Future, yanayolenga kuhamasisha ulimwengu juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi na kuongeza uelewa kuhusiana na ongezeko la joto duniani na rasilimali zinginezo duniani.

Maelfu ya miji yamefanya matamasha na maonesho katika kuhamasisha hatua stahiki kwenye kuzuia mabadiliko ya tabia nchi, na maandamano ya haki za vijana kuhusu kizazi kijacho[1]. Kwa takwimu za matamasha, washiriki walikuwa kama ifuatavyo[2]: nchi 154, miji 2362, na matamasha 3615. Pia, iliripotiwa idadi ya washiriki ilikuwa chini kufuatia kanuni za Uviko[3].

Marejeo hariri

  1. Solheim, Erik (2020-01-02). "Interview with Erik Solheim on Global Climate Action Day, 25 September 2020". Scottish Geographical Journal 136 (1-4): 112–117. ISSN 1470-2541. doi:10.1080/14702541.2020.1856094. 
  2. dx.doi.org http://dx.doi.org/10.12952/journal.elementa.000107.s007. Iliwekwa mnamo 2022-05-07.  Missing or empty |title= (help)
  3. "Greenpeace calls for urgent global action to save The Great Northern Forest". Climate Change and Law Collection. Iliwekwa mnamo 2022-05-07.