Sogea Karibu ni jina la wimbo wa muziki wa dansi uliotungwa na Kakere Belesa na kuimbwa na Hassan Bitchuka kwa ajili ya Juwata Jazz Band mnamo 1979. Wimbo huu unasifika sana kwa kinanda (organ) chake cha huzuni kilichopigwa na mpigaji nguli wa "The Kilimanjaro Band", Waziri Ally (Kissinger). Sababu zilizopelekea kupiga organ katika wimbo huu, ni kuwa wapigaji wa vyombo vya upepo waligoma (tarumbeta na sax) kwa kuuona wimbo ni mbaya. Lakini baada ya kutoka wote walishangazwa na utamu uliopatikana katika wimbo huu. Sauti kuu ya wimbo huu imeimbwa na Hassan Rehani Bitchuka kwa ustadi wa hali ya juu. Ni moja kati ya nyimbo zilizotamba sana za Juwata Jazz Band kwa kipindi cha miaka ya 1970 na 1980 mwanzoni.

"Sogea Karibu"
Wimbo wa Juwata Jazz Band

kutoka katika albamu ya Mpenzi Zarina

Umetolewa 1979
Umerekodiwa 1979
Aina ya wimbo Muziki wa dansi
Lugha Kiswahili
Urefu 8:48
Studio RTD
Mtunzi Kakere Belesa
Mtayarishaji Juwata Jazz Band
Mpenzi Zarina orodha ya nyimbo
  1. SideA1 Mpenzi Zarina
  2. SideA2 Mwana Wacha Wizi
  3. SideA3 Uzuri Si Shani
  4. SideA4 Epuka Tabia Mbaya
  5. SideB1 Sogea Karibu
  6. SideB2 Vijana Tujitokeze
  7. SideB3 Selemani
  8. SideB4 Talaka

Wimbo unahusu mke mwema aliyekuja kubadilika tabia zisizovumilika katika ndoa. Mwishowe anamtaka abebe kilicho chake heri abaki mwenyewe. Wimbo umeimbwa kwa huzuni wa hali juu kabisa kwa muziki wa dansi wa kipindi hiko. Wimbo huuu ulikuwa utunzi wa Kakere Belesa, Kakere na Bitchuka walikuwa wanaishi nyumba moja ya kupanga miaka hiyo, Kakere alipompa Bitchuka wimbo huu, Bitchuka akafanya marekebisho madogo hasa yale maneno ya mwanzoni mwa wimbo sogea karibu Kakere alikuwa anaimba, Bitchuka akapendekeza heri iwe ya kuongea badala ya kuimba.

Baada ya hatua hiyo kwisha, wakaupeleka kwa wenzao ili wauanzie mazoezi, lakini watu wa ala za upepo chini ya uongozi wa Joseph Lusungu waliususia wimbo huu. Lakini baada ya kutoka wote waliukubali. Licha ya uwezo mkubwa wa Kakere wa kuimba, bado aliona wimbo huu ampatie sahib wake. Hii inadhihilisha ya kwamba wasanii wa zamani hawakuwa na choyo katika kufikisha ujumbe kwa hadhira husika. Uwezo wa Kakere unaweza kuusikia katika wimbo kama vile Asia, Chande, Baby Wangu - zote akiwa Bima.

Tazama pia hariri

Viungo vya Nje hariri