Elimujamii

(Elekezwa kutoka Sosholojia)

Elimujamii ni fani ya sayansi inayochunguza mwenendo wa kijamii, yaani binadamu katika maisha ya jamii: unavyoanza, unayoendelea, unavyojipanga na unavyosababisha miundo.[1]

Mwana elimujamii Auguste Comte (1798-1857).

Kwa maneno mengine, elimujamii inamsoma mtu katika mahusiano yake: mtu na mtu, mtu na watu (kundi) na hivyo huweza kugundua tabia zake mbalimbali.

Somo hilo linahusiana na masomo mengine, kama vile anthropolojia, historia, elimunafsia na uchumi.

Ni mojawapo kati ya sayansi za jamii nayo inatumia mbinu tofauti za kutambua hali halisi, halafu inazichunguza kimpango.

Jina la fani hii linatokana na Kilatini ("socius" yaani "mwenzi") na Kigiriki ("λογία, logia" yaani "elimu") pamoja.

Aliyeunganisha kwa mara ya kwanza maneno hayo (mwaka 1780) ni mwandishi Mfaransa Emmanuel-Joseph Sieyès (17481836), lakini alichoandika kilichelewa kuchapwa.[2] Mwaka 1838 alifanya vilevile Mfaransa mwingine, mwanafalsafa wa sayansi Auguste Comte (17981857).[3] Comte used this term to describe a new way of looking at society.[4]

Faida ya fani hii

hariri

Kujifunza elimujamii ni kujifunza kuangalia dunia kwa mapana zaidi, yaani kutoka nje ya mipaka ya tafsiri zetu tulizojiwekea kijuujuu. Ni kukubali changamoto ya kuchunguza upya yale yote tunayoyajua kwa maana za kawaida: matokeo ya uchunguzi huo pengine hupingana na kile tulichokidhani mwanzoni na hivyo kutuwezesha kuuona ukweli katika hali mpya.

Elimujamii hutusaidia kuelewa hali halisi ya jamii ili kuchangia urekebishaji au utengenezaji wa sera mpya. Hutusaidia pia kukuza ujuzi wetu wa jamii mbalimbali na wa mahusiano yetu kijamii, yakiwa mazuri au mabaya vilevile. Hutusaidia tena kuelewa jumuia zetu kubwa au ndogo kama watu wanaoishi pamoja wakifuata mila na desturi za aina moja na kuwa na lengo moja. Hutusaidia kuelewa aina mbalimbali za utamaduni ili kurahisisha ushirikiano.

Historia ya elimujamii

hariri

Pamoja na kwamba mizizi ya elimujamii inapatikana katika maandishi ya wanafalsafa wa Ugiriki Plato na Aristotle, somo hilo lilipata kujitegemea katika karne ya 19 likakua haraka katika karne ya 20.

Mababa wake ni hasa Auguste Comte (1798-1857) na Herbert Spencer (1820-1903).

Wengineo ni Karl Marx (1818-1883), Emile Durkheim (1858-1917) na Max Weber (1864-1920).

Tanbihi

hariri
  1. sociology. (n.d.). The American Heritage Science Dictionary. Retrieved July 13, 2013, from Dictionary.com website: http://dictionary.reference.com/browse/sociology
  2. Des Manuscrits de Sieyès. 1773–1799, Volumes I and II, published by Christine Fauré, Jacques Guilhaumou, Jacques Vallier and Françoise Weil, Paris, Champion, 1999 and 2007. See also Christine Fauré and Jacques Guilhaumou, Sieyès et le non-dit de la sociologie: du mot à la chose, in Revue d'histoire des sciences humaines, Numéro 15, novembre 2006: Naissances de la science sociale. See also the article 'sociologie' in the French-language Wikipedia.
  3. A Dictionary of Sociology, Article: Comte, Auguste
  4. Macionis, Gerber, John, Linda (2010). Sociology 7th Canadian Ed. Toronto, Ontario: Pearson Canada. pp. 10.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
Vyama vya taaluma hii
Vyanzo vingine
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elimujamii kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.