Standard English-Swahili Dictionary
Madan-Johnson's Standard English-Swahili Dictionary (kifupi: M-J SES) iliandaliwa na wataalamu wa "Inter-territorial Language (Swahili) committee to the East African Dependencies" baada ya Vita Kuu ya Kwanza kwa ajili ya maeneo chini ya utawala wa Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Kamati iliandaa kamusi mbili za Kiingereza-Kiswahili na pia Kiswahili-Kiingereza (M-J SSE).
Mhariri Mkuu wa kamati alikuwa katibu yake Frederick Johnson. Msingi wa kamusi hizi ulikuwa kazi ya A. C. Madan. Hivyo kamusi hizi hutajwa kama "Madan-Johnson".
Mara nyingi lugha ya kamusi hizi si tena Kiswahili cha kisasa. Lakini zimeendelea kuchapishwa mara nyingi hadi wakati wa kisasa.
Marejeo
hariri- Madan-Johnson, A Standard English-Swahili Dictionary (hutolewa na Oxford University Press, Nairobi & Dar es Salaam, 1939 na kuchapishwa upya mara nyingi)