Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z. ni jina la kutaja albamu ya pili ya rapa wa West Coast 2Pac. Hii ipo sawa tu na ile ya kwanza, 2Pacalypse Now, albamu ina nyimbo kibao za 2Pac zinazosisitiza mitazamo ya kijamii na siasa kwa ujumla. Albamu ilitakiwa iitwe "Troublesome 21", hiyo 21 inataja umri wa Shakur kwa kipindi hicho. "N.I.G.G.A.Z." inasimama kama "Never Ignorant Getting Goals Accomplished." Yaani "Mjinga Kamwe Hafanikishi Malengo."
Ilivyotoka tu ikaingia #24 kwenye chati za Billboard 200, albamu hii imeona zaidi mafanikio kuliko hata ile iliotangulia, na kuna tofauti kibao katika utayarishaji ambazo zinaelezeka. Vibao kikali kutoka kwenye albamu hii ni "Keep Ya Head Up" na "I Get Around" na zimefika kiwango cha platinum. Ingawa albamu yenyewe kabisa ilitolewa chini ya Interscope, haki zote kwa sasa zinamilikiwa na Amaru Entertainment, studio inayomilikiwa na Afeni Shakur, mama yake rapa huyu.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z. kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.