Usufii

(Elekezwa kutoka Sufii)

Usufii (kar. صوفی sufi) pia tasawuf (kar. تصوف ) au Uislamu wa Kisufii ni tawi la Uislamu linalotafuta maarifa ya moyoni kuhusu ya Mungu na imani.

Sufi (dervish) jinsi anavyocheza mbele ya msikiti huko Omdurman, Sudan

Wafuasi wa mwelekeo huu wanaweza kuitwa Sufii, Dervish au Fakir.

Wasufii wanaamini ya kwamba inawezekana kumkaribia Mungu katika maisha ya sasa kabla ya kifo wakielekea kuungana na nuru au roho ya Allah iwezekanavyo.

Wanakazia kutawala fikra na tamaa za kimwili na kuondoa kila kitu ndani ya nafsi kisicholingana na Mungu. Kwa njia hii walimu wao wanafundisha kuna uwezekano kuachana na nafsi kabisa na kusikia umoja na Mungu.

Wasufii wengi hukazia upendo wa Mungu na upendo kwa Mungu.

Kwa kukaribia shabaha hii Wasufii wengine wanafundisha maisha ya kuachana na dunia na tamaa na mambo yake yote. Hapo wanaweza kufanana na watawa katika dini nyingine kama vile Wakristo au Wahindu ingawa hawajui amri ya useja au kutooa.

Tarika

hariri

Wasufii wengi wameungana katika jumuiya mbalimbali zinazoitwa "tarika" (kar. طريقة - "njia") na jumuiya hizi hufuata maagizo wa kiongozi (mara nyingi mwenye cheo cha sheikh) aliyeiunda.

Wanakutana kwa mazoezi ya kiroho na haya ni pamoja na dhikr (kumbukumbu kwa Mungu kwa njia ya kurudiarudia jina Allah au majina yake mengine), uimbaji na kucheza. Sehemu ya Wasufii wanatumia aina ya kucheza ambako kila mshiriki anazunguka kiduara.

Kati ya jumuiya makubwa ya Wasufi ni

Wasufi mashuhuri

hariri

Kati ya Wasufii waliokuwa mashuhuri ni wafuatao:

Usufi na Uislamu rasmi

hariri

Mazoezi ya Wasufi hazikubaliki na sehemu za Waislamu wengine. Wasufi wameshtakiwa kutembea nje ya Uislamu.

Hasa mielekeo makali kama Wahabiya au Salafiya imepinga Wasufii na kuwashambulia pale walipo na nguvu au mamlaka. Siku hizi nyumba na mikutano ya Wasufi zimeshambuliwa hasa nchini Pakistan.[2]. Kiongozi wao Riaz Ahmed Gohar Shahi na vitabu vyake vimepigwa marufuku na wafuasi wanaojulikana wanakamatwa. [3].

Nchini Saudia wataalamu wa kidini wa serikali walitangaza Usufii kuwa shirk lakini miaka ya nyumba kuna taarifa ya nafasi kubwa zaidi kwa wafuasi wa Usufii kuwa na mikutano.[4]

Nchini Uajemi (Iran) serikali inajaribu pia kuwafuata Wasufii kwa kufunga nyumba zao. [5].

Kinyume chake mkutano wa kimataifa wa wataalamu waislamu nchini Jordan ilitangaza mwaka 2005 kuwa Usufi ni tawi halali la Uislamu. [6].

Kujisomea

hariri
  • Abu-Nasr, J (2007) Muslim Communities of Grace:Sufi Brotherhoods in Islam London;
  • Burckhardt, T (1963) An Introduction to Sufi Doctrine Lahore;
  • Godlas, A (2000) Sufism's Many Paths U of Georgia Press;
  • Shah, Idries (1971) The Sufis New York;
  • Schimmel, A (1983) Mystical Dimensions of Islam Chapel Hill: U of North Carolina Press;
  • Smoley, Richard & Kinney, Jay. 2006. Hidden wisdom: a guide to the western inner traditions. 2nd ed; Wheaton, Illinois: Quest Books. ISBN 978-0-8356-0844-2 (Chapter 10 deals with Sufism in the West)

Marejeo

hariri
  1. "The Meccan Revelations". World Digital Library. 1900–1999. Iliwekwa mnamo 2013-07-14.{{cite web}}: CS1 maint: date format (link)
  2. The Daily Times Lahore, Pakistan, 8 July 2004
  3. http://www.dawn.com/2002/06/26/nat33.htm Daily Dawn Karachi, Pakistan, news item, 26 June 2002, Retrieved 2 Nov 2012
  4. In Saudi Arabia, a Resurgence of Sufism; taarifa ya Washington Post 2006
  5. See US Report on International Religious Freedom May 2009, Section on Iran
  6. http://ammanmessage.com/ The Amman Message Summary Retrieved 2 Nov 2012