Sulfacetamide
Sulfacetamide ni antibiotiki inayotumika kutibu kuvimba utando wa nje kwenye mboni ya jicho na kope la ndani kutokana na bakteria, chunusi, na ugonjwa wa ngozi wa seborrheic.[1][2] Ingawa imetumika kwa trakoma, antibiotiki zinazotumiwa kwa njia ya mdomo pia zinahitajika.[1] Dawa hii inapakwa kwenye ngozi, au kama matone ya jicho au dawa ya kupaka ya macho.[2][1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwasha na kuumwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[1] Matumizi yake ya muda mrefu yanaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa na kuvu.[1] Dawa hii ni katika dawa zulfanamidi zinazotumika kutibu maambukizi ya bakteria (sulfonamide).[1]
Sulfacetamide iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1946.[1] Nchini Marekani, chupa ya mililita 15 za matone ya macho hugharimu takriban dola 20 za Marekani, huku chupa ya mililita 118 ya mafuta ya ngozi ikigharimu takriban dola 50 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[3][4]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Sulfacetamide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "Klaron medical facts from Drugs.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-24. Iliwekwa mnamo 2021-02-24.
- ↑ "Sulfacetamide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sulfacetamide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sulfacetamide kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |