Sven Constantin Voelpel
Makala hii au sehemu ya makala hii inahitaji masahihisho kwa upande mmoja wa zifuatazo:
|
Sven Constantin Voelpel (amezaliwa 13 Oktoba, 1973 mjini Munich) ni mtaalamu nadharia shirika Ujerumani na Profesa wa Usimamizi wa Biashara katika shule ya Utu na Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Jacobs University Bremen nchini Ujerumani. Anajulikana kwa kazi yake katika uwanja wa kumudu mikakati, miundo ya biashara [1] na kumudu maarifa [2].
Wasifu
haririVoelpel alipokea shahada yake ya uzamili katika Uchumi, Sayansi za Jamii na Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo kikuu cha University of Augsburg mwaka wa 1999 na shahada yake ya PhD katika Usimamizi wa biashara kutoka chuo kikuu cha University of St. Gallen mwaka wa 2002 nchini Uswizi. [3]
Voelpel alianza kazi yake ya kitaaluma kama Post-Graduate katika chuo kikuu cha Harvard University mwaka wa 2002 nchini Amerika na akaendelea na utafiti wake katika chuo kikuu cha Oxford University mwaka wa 2008.Mnamo mwaka wa 2003-2004 alikuwa Profesa mshirika katika Chuo kikuu cha University of Groningen na katika chuo kikuu cha Norwegian School of Economics. Mwaka wa 2004 alihamia chuo kikuu cha Jacobs University Bremen ambapo aliteuliwa kama Profesa wa Usimamizi wa Biashara. [3]
Mwaka wa 2007 Voelpel alianzisha WDN- WISE Demographics Network Bremen Ujerumani na amekuwa mkurugenzi wake tangu kuanzishwa.WDN hutoa suluhu maalum za kisayansi kwa kampuni zinazoshirikiana nayo.Suluhu hizi zinashughulikia maswala yanayohusiana na demografia ya wafanyakazi.
Voelpel alikuwa mshiriki wa bodi ya wahariri katika jarida la Journal of Change Management (2004-2010), na Journal of Knowledge Management (2004-2006).Tangu mwaka wa 2008 hadi hivi sasa amekuwa mshiriki wa bodi ya wahariri katika jarida la Organization Studies (Journal).
Kazi
haririUtafiti wa Voelpel unazingatia maswala katika nyanja za uongozi,ufanisi wa timu,usimamizi wa maarifa [4] na usimamizi wa mabadiliko na demografia [5][6] na usimamizi wa utofauti. [4]
Makala yake “The rise of knowledge towards attention management“ yametambuliwa kama mojawapo ya makala yenye kiwango cha juu katika uwanja wa usimamizi wa maarifa [7] kutokana na idadi nyingi ya kurejelewa yamepokea katika uandishi wa makala mengine. Mwaka wa 2009 na 2012 aliorodheshwa kama mmojawapo wa watafiti 100 bora wenye umri wa chini ya 40 [8][9] na Handelsblatt. Katika tija ya binafsi aliorodheshwa katika nafasi ya 33 na KM/IC researchers. [10]
Kama mkurugenzi mwanzilishi wa WDN Archived 24 Januari 2021 at the Wayback Machine. utafiti wa Voelpel katika uongozi wa demographia umekuwa ukishawishi vyema mazingira ya kazi ya mamilioni ya wafanyakazi katika kampuni zinazoshirikiana na WDN.Baadhi ya kampuni hizi ni Daimler AG, Deutsche Bahn, na Deutsche Bank miongoni mwa zingine [11].Mwaka wa 2013 WDN ilianzisha programu ya mashindano kwa jina "Intergenerational Competence and Qualification Program Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.",yaliyofanywa na Federal Ministry of Education and Research (Germany) (BMBF) “ ili kutafuta suluhu mwafaka kwa mabadiliko ya demographia katika utendakazi. [12]
Kitabu chake kilichochapishwa hivi karibuni, Mentale, emotionale und körperliche Fitness kimedhihirisha utafiti wake juu ya ustawi na ufanisi binafsi wa watu. Kitabu hiki kimepokea maoni chanya juu katika Magazin für Gesundheit und Wohlbefinden – Gesund … katika gazeti la Die Zeit na kuchapishwa katika nakala 650,000. [13]
Baadhi ya Makala Aliyoandika
hariri- Biemann, T., Cole, M.S. & Voelpel, S.C.: Within-group agreement: On the use (and misuse) of rWG and rWG(J) in leadership research and some best practice guidelines. Leadership Quarterly, 23(1), 66-80, 2012.
- Kearney, E., Gebert, D. & Voelpel, S.C.: When and how diversity benefits teams: the importance of team members need for cognition. Academy of Management Journal, 52(3), 581-598, 2009.
- Voelpel, S.C., Eckhoff, R., & Förster, J.: David against Goliath? Group size and bystander effects in virtual knowledge sharing. Human Relations, 61(2), 273-297, 2008.
- Nonaka, I., von Krogh, G., & Voelpel, S.C.: Organizational knowledge creation theory: Evolutionary paths and future advances. Organization Studies, 27(8), 1179–1208, 2006.
- Voelpel, S.C., Dous, M., & Davenport, T.:. Five steps to creating a global knowledge sharing system: Siemens Share-Net. Academy of Management Executive, 19(2), 9-23, 2005.
Baadhi ya Vitabu Alivyoandika
hariri- Davenport, T., Leibold, M., & Voelpel, S. (2006). Strategic management in the innovation economy. Strategy approaches and tools for dynamic innovation capabilities. New York: Wiley (Utangulizi kutoka kwa Klaus Jacobs,na Heinrich von Pierer; Vorstandsvorsitzender der Siemens AG) ISBN 978-3-89578-263-3
- Leibold, M., & Voelpel, S. (2006). Managing the aging workforce: Challenges and solutions. New York: Wiley (Utangulizi kutoka kwa Heinrich von Pierer na Klaus Jacobs). ISBN 978-3-89578-284-8
- Voelpel, S. & Lanwehr, R. (2009). Management für die Champions League. Was wir vom Profifußball lernen können. Erlangen – New York: Publicis ( Pamoja na mahojiano na Jörg Wontorra na utangulizi kutoka kwa Roland Berger). ISBN 3-89578-290-4
- Voelpel, S., Leibold, M., & Früchtenicht, J.-D. (2007). Herausforderung 50 plus: Konzepte zum Management der Aging Workforce: Die Antwort auf das demographische Dilemma. Erlangen – New York: Publicis-Wiley (Utangulizi kutoka kwa Heinrich von Pierer na Klaus Jacobs). ISBN 978-3-89578-291-6
Marejeo
hariri- ↑ Wirtz, Bernd W., Oliver Schilke, and Sebastian Ullrich. "Strategic development of business models: implications of the Web 2.0 for creating value on the internet." Long Range Planning 43.2 (2010): 272-290.
- ↑ Tsoukas, Haridimos. "A dialogical approach to the creation of new knowledge in organizations." Organization Science 20.6 (2009): 941-957.
- ↑ 3.0 3.1 "Sven Voelpel, Professor of Business Administration at Jacobs University Bremen," linkedin profile, 2015
- ↑ 4.0 4.1 Bamberger, P. A., Biron, M., & Meshoulam, I. (2014). Human resource strategy: Formulation, implementation, and impact. Routledge. pp.212
- ↑ "Völlig unentbehrlich". Zeit. 2011. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bruch, H., Kunze, F., & Böhm, S. (2009). Generationen erfolgreich führen: Konzepte und Praxiserfahrungen zum Management des demographischen Wandels. Springer-Verlag.
- ↑ Serenko, Alexander; Dumay, John (2015). "Citation classics published in knowledge management journals. Part I: articles and their characteristics". JOURNAL OF KNOWLEDGE MANAGEMENT. 19 (2): 428.
{{cite journal}}
:|access-date=
requires|url=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Handelsblatt Ranking Betriebswirtschaftslehre 2009". Handelsblatt. Handelsblatt. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-27. Iliwekwa mnamo 29 Januari 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Handelsblatt Ranking Betriebswirtschaftslehre 2012". Handelsblatt. Handelsblatt. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-13. Iliwekwa mnamo 30 Januari 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Meta-Review of Knowledge Management and Intellectual Capital Literature: Citation Impact and Research Productivity Rankings". Wiley InterScience. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Netzwerk wappnet sich für den demografischen Wandel". Bremen Digital Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-29. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Land der demografischen Chancen". Die Demografische Chance. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-29. Iliwekwa mnamo 26 Aprili 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mentale, emotionale und körperliche Fitness". Magazin für Gesundheit und Wohlbefinden – Gesund …, Die Zeit (kwa German) (42): 18. 9 Oktoba 2014.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Tovuti
hariri- Tovuti Rasmi ya Sven Voelpel
- Tawasifu ya Sven C. Voelpel Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.,Jacobs University Bremen
- WISE Research Group Archived 10 Agosti 2018 at the Wayback Machine.
- WDN – WISE Demographie Netzwerk