Syngas
Syngas, au gesi ya awali, ni mchanganyiko wa hidrojeni na monoksidi kaboni, katika uwiano mbalimbali. Gesi hii mara nyingi huwa na kaboni dioksidi na methane na hutumika kutengeneza amonia au methanoli.
Syngas inaweza kuwaka na inaweza kutumika kama mafuta.
Kihistoria, imekuwa ikitumika kama mbadala wa petroli, wakati usambazaji wa petroli umepunguzwa; kwa mfano, gesi ya kuni ilitumiwa kuendesha magari huko Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (huko Ujerumani pekee magari nusu milioni yalijengwa au kujengwa upya kuwezeshwa na gesi ya kuni).
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Syngas kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |