Taasisi ya Madini na Teknolojia ya Namibia
Taasi ya Namibia ya Madini na Teknolojia (NIMT) ni taasisi ya mafunzo ya kitaalamu ya ufundi iliyopo Arandis, Namibia, iliyoanzishwa mnamo 1991. Ilikuwa na wanafunzi 4,000 na wafanyakazi 270 mnamo 2017, Eckhart Mueller alikuwa mkurugenzi mtendaji wake hadi alipouawa pamoja na naibu wake mnamo 15 Aprili 2019. NIMT inatoa kozi katika madini, utengenezaji na uhandisi.
Mnamo 2007, De Beers ilitoa N$2.1 milioni kufungua kampasi ya pili kaskazini na mnamo Novemba mwaka huo kampasi ilifunguliwa Tsumeb. NIMT pia inaendesha kampasi katika Keetmanshoop kusini mwa Namibia.[1]
NIMT hutoa kati ya wahitimu 300 na 500 kwa mwaka ambao huajiriwa na sekta ya madini ya Namibia.[2]
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Taasisi ya Madini na Teknolojia ya Namibia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |