Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ni taasisi ya umma iliyopo Arusha, Tanzania.[1] Ni moja kati ya Taasisi za Sayansi na Teknolojia zilizopo katika bara la Afrika. NM-AIST Arusha, imesajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na ni taasisi ya utafiti wa kina wa masomo katika ngazi ya uzamili, uzamifu na utafiti katika Sayansi ya Uhandisi na Teknolojia (SET). Mafunzo ya SET, yanajumuisha kipimo cha mafunzo ya kibinadamu na viungo vya masomo ya biashara. Sayansi ya maisha na uhandisi wa kibayolojia inaendelezwa ili kuwa mojawapo ya maeneo muhimu ya NM-AIST Arusha, ikichukua fursa mbalimbali ya kibayolojia katika Mkoa. Hivyo basi, taasisi inalenga kuchochea, kukuza na uimarishaji wa uzalishaji wa kilimo, na kuongeza thamani ya bidhaa mbalimbali za asili (yaani kilimo, madini, n.k.) yanayozalishwa nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki. Maeneo mengine makuu yatakayoshughulikiwa na NM AIST-Arusha ni pamoja na Nishati, ICT, Madini, Mazingira na Maji.[2]
Marejeo
hariri- ↑ "Register of Universities" (PDF). Tanzania Commission for Universities. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 24 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 15 Julai 2013.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help) - ↑ "Nelson Mandela African Institute of Science and Technology".