Tafamidisi, inayouzwa kwa jina la chapa Vyndaqel miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibuu ugonjwa adimu unaoendelea unaosababishwa na mkunjo usio sahihi wa protini inayoitwa transthyretin, ambayo kwa kawaida husaidia kusafirisha homoni ya tezi na vitamini A katika mkondo wa damu (transthyretin-mediated amyloidosis).[1] Dawa hii inachukuliwa kwa njia ya mdomo.[2] Inaweza kusimamishwa baada ya upandikizaji wa ini.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuhara, na maambukizi.[2] Inaaminika kuwa matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[3] Dawa hii inafanya kazi kwa kuleta utulivu wa protini ya transthyretin, kwa hivyo kupunguza uundaji wa amiloidi.[4]

Tafamidisi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu barani Ulaya mwaka wa 2011 na Marekani mwaka wa 2019.[4][1] Nchini Uingereza, matumizi ya miligramu 20 kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £10,700 kufikia mwaka wa 2021.[2] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 4,900 za Marekani.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Tafamidis Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 428. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)
  3. "Tafamidis Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Vyndaqel EPAR". European Medicines Agency (EMA). 16 Oktoba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Vyndaqel Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tafamidisi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.