Jina Taifa la Mungu linatumika katika Biblia kumaanisha kwanza taifa la Israeli. Baadaye, Wakristo walilitumia kwa ajili yao katika Agano Jipya kama warithi wa wito wa taifa hilo kupitia Yesu Kristo na Mitume wake 12.

Katika Biblia hariri

Jina linapatikana katika Waamuzi 20:2; Kitabu cha Pili cha Samueli 14:13; Kitabu cha Esta 10:10; Waraka kwa Waebrania 4:9; 11:25; Waraka wa pili wa Petro 2:10.

Pamoja na hayo, wazo linajitokeza katika Injili ya Mathayo 21:43; Ufunuo wa Yohane 5:9; 21:3.

Katika imani na teolojia hariri

Kanisa lilianza kulitumia tena kutokana na juhudi za wataalamu wa Biblia wa karne ya 20.

Kanisa Katoliki lilitumia rasmi hasa katika hati za Mtaguso wa pili wa Vatikano, hususan Lumen Gentium sura yote ya pili. Humo, baada ya ile ya kwanza kueleza fumbo la Kanisa, inaelezwa kuwa fumbo hilo katika historia linajitokeza kama taifa, kwa kuwa tangu awali Mungu hakupenda kuokoa binadamu mmojammoja, bali kwa mshikamano. Taifa hilo moja linatokana sasa na mataifa yote na kulenga kuyaunganisha ndani ya Yesu, mfalme wake.