Kwa Tairi kama jina la nyota inayoitwa kwa Kiingereza Altair angalia hapa Tairi (nyota)

Matairi ya magari

Tairi (kutoka Kiingereza en:tyre) ni sehemu ya nje ya gurudumu. Hapo tunatofautisha rimu na tairi ilhali rimu ni sehemu ya ndani ya gurudumu.

Kwa kawaida tairi hutengenezwa kwa mpira au dutu nyingine nyumbufu. Mara nyingi tairi huwa na nafasi ndani yake inayojaa hewa yenye shinikizo la juu. Hivyo tairi inaweza kusharabu mishtuko kutokana na mashimo au miinuko njiani na hivyo kuleta mwendo nyororo wa gari.

Uso wa nje wa tairi una tredi maana yake kuna mifereji na matuta madogo yenye kazi ya kuboresha tabia za kulenga na kutoteleza kwenye uso wa njia.

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: