Tamasha la Adae
Tamasha la Adae ni sherehe inayoadhimishwa katika Mkoa wa Ashanti. Inachukuliwa kama siku ya kupumzika, na ni desturi ya zamani sana ya kihistoria ya watu wa Ashanti.
Kutekelezwa
haririNdani ya mzunguko wa wiki sita, Adae ina siku mbili za sherehe, mara moja Jumapili (Akwasidae) na tena Jumatano (Awukudae). Mzunguko wa Adae unarudiwa mara tisa katika mwaka mmoja. Kulingana na kalenda ya Akan, Tamasha la Adae la tisa, linaloitwa Tamasha la Adae Kese (Adae kubwa), hutokea wakati wa sherehe ya Mwaka Mpya. Kwa hivyo, sherehe hii hufanyika kushukuru miungu na mababu kwa mavuno mapya.[1] Matamasha ndani ya Adae hayawezi kubadilishwa badilishwa, kwa sababu yalifungwa tangu enzi za kale.
Marejeo
haririMakala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
- ↑ Asante, Molefi Kete; Mazama, Ama (26 Novemba 2008). Encyclopedia of African Religion. SAGE. ku. 36–. ISBN 978-1-4129-3636-1. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2012.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu Ghana bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |