Tamasha la Sanaa na Vitabu la Aké
Tamasha la Sanaa na Vitabu la Aké ni tukio la fasihi na sanaa linalofanyika kila mwaka nchini Nigeria. Lilianzishwa mwaka 2013 na Lola Shoneyin, mwandishi na mshairi wa Nigeria, huko Abeokuta. Linajumuisha waandishi wapya na walio na uzoefu kutoka kote ulimwenguni na lengo lake kuu limekuwa kukuza, kuendeleza na kusherehekea ubunifu wa waandishi, washairi na wasanii wa Kiafrika. Tamasha la Sanaa na Vitabu la Aké limeelezewa kama mkusanyiko mkubwa zaidi wa kila mwaka wa waandishi wa fasihi, wahariri, wakosoaji na wasomaji barani Afrika.[1] Tamasha hili lina tovuti rasmi na jarida maalumu, linalojulikana kama Aké Review.[2]
Marejeo
hariri- ↑ Obi-Young, Otosirieze (23 Juni 2018). "Fantastical Futures | Ake Festival 2018 Will Focus on a Re-Imagined Africa". Brittle Paper.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Lola Shoneyin (9 Januari 2015). "Why I organise annual Ake Arts and Book Festival". Newswatch Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Mei 2016. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tamasha la Sanaa na Vitabu la Aké kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |