Tangi
Tangi ni chombo kikubwa kinachotumiwa kuhifadhia au kuwekea vimiminika au gesi[1]. Hutengenezwa kwa bati gumu, chuma, plastiki au dutu nyingine isiyoathirika na vitu vinavyohifadhiwa mle.
Tangi zinapatikana kwa maumbo tofauti na kila ukubwa. Tangi ndogo mfano ya kibatari hushika mafuta kidogo kama nusu thumuni ya lita, tangi la gari huwa na lita 50-60 na matangi makubwa yanayopatikana bandarini hushika lita milioni kadhaa yakipokea mafuta kutoka meli zinazobeba mafuta[2].
Marejeo
hariri- ↑ linganisha KKS3, uk. 550 "tangi"
- ↑ linganisha [https://shipnext.com/port/582473d8c9c19c0be8d8cb92 Rotterdam (Netherlands), General Description] Archived 22 Machi 2023 at the Wayback Machine., tovuti ya shipnext.com, iliangaliwa MAchi 2023