Tasimelteon, inayouzwa kwa jina la chapa Hetlioz miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa kuamka kwa saa 24.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo, saa moja kabla ya kulala.[1][2] Manufaa yake yanaweza kuchukua miezi kadhaa kutokea.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuhisi usingizi, kichefuchefu na kizunguzungu.[2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii inafanya kazi kwa kuwezesha kipokezi cha melatonin.[2]

Tasimelteon iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2014 na Ulaya mwaka wa 2015.[1][2] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 23,000 za Marekani kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[3] Licha ya kuidhinishwa barani Ulaya na kupatikana nchini Ujerumani haijauzwa nchini Uingereza kufikia mwaka wa 2021.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Tasimelteon Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Hetlioz EPAR". European Medicines Agency (EMA). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 2 Desemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Hetlioz Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Tasimelteon". SPS - Specialist Pharmacy Service. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tasimelteon kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.