Tatiana Vivienne
Tatiana "Tati" Vivienne ni mtetezi wa haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ndiye mwanzilishi na mkurugenzi wa Femmes Hommes Action Plus (FHAP), shirika linalolenga kusaidia wanawake na wasichana waliotengwa zaidi na waliopatwa na kiwewe.
Maisha ya mwanzo
haririTatiana Vivienne alikulia kwenye ukingo wa Bangui, mmoja kati ya watoto kumi, mabinti wanne na wavulana sita. Akiwa na umri wa miaka mitano hivi, baba yake alilazimika kuhamia Baboua, kaskazini-magharibi mwa nchi, kwa ajili ya kazi, naye akasomeshwa huko katika shule ya Kanisa Katoliki. Kwa sababu ya ukosefu wa utulivu huko CAR wakati huo, wazazi wake, ambao waliamini umuhimu wa elimu bora, walilazimika kumpeleka Afrika Magharibi ili kukamilisha masomo yake.
Harakati
haririBaada ya kukutana na wanawake na watoto ambao walikuwa wakilengwa na Lord's Resistance Army (LRA), Vivienne alianzisha Femmes Hommes Action Plus (FHAP) mnamo mwaka 2011. FHAP inalenga katika kuwasaidia wasiojiweza zaidi, wasichana na wanawake wachanga ambao wametelekezwa na pia husaidia kuwaunganisha tena wanawake katika jumuiya zao ikiwa ni pamoja na wale ambao wametoroka kutoka kwa LRA. Akizungumzia kuhusu FHAP Vivienne amesema: "Sisi ni sauti kwa wasio na sauti." Shirika lake ni mojawapo ya machache yanayofuatilia kuweka kumbukumbu na kuripoti ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na (LRA) katika eneo la Mashariki. FHAP pia inatoa usaidizi wa kisheria na kisaikolojia kwa waathiriwa.Amekumbana na matatizo na changamoto nyingi katika kuendesha FHAP, ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kufunga ofisi ya Bangui, wizi wa nyumba yake kwa kutumia silaha pamoja na uhaba wa fedha wa kudumu.
Maisha binafsi
haririVivienne anaishi Bangui, "karibu na familia yake kubwa".