Tekle Giyorgis II (alifariki 1872) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 11 Juni 1868 hadi 11 Julai 1871. Alimfuata Tewodros II. Jina lake la kubatizwa lilikuwa Wagshum Gobeze. Kwa vile alikuwa mrithi wa nasaba ya Zagwe (upande wa baba yake) na mama yake alikuwa binti wa nasaba ya Solomoni, alijitangaza mfalme mkuu baada ya kifo chake Tewodros II. Utawala wake ulikuwa mfupi tu. Alishindwa katika mapigano na kukamatwa na Dejazmach Kassa aliyemfuata kama mfalme chini ya jina la Yohannes IV. Tekle Giyorgis II alifariki kifungoni baada ya mwaka mmoja tu.

Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tekle Giyorgis II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.