Tesamorelin, inayouzwa kwa jina la chapa Egrifta, ni dawa inayotumika kutibu lipodystrophy inayohusishwa na HIV.[1] Hasa hutumiwa kwa mafuta ya ziada ya tumbo[2] na inatolewa kwa sindano chini ya ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya viungo, uwekundu kwenye sehemu ya sindano na uvimbe wa mguu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio na saratani.[1] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[1] Dawa hii ni aina iliyotengenezwa ya homoni inayochochea kutolewa kwa homoni ya ukuaji (kutoka kwenye tezi ya pituitari) katika Kiingereza (growth-hormone-releasing hormone).[1]

Tesamorelin iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2010[1] lakini haijaidhinishwa huko Uropa.[2] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 6,400 za Marekani kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Tesamorelin". drugs.com. American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 1 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Egrifta: Withdrawal of the marketing authorisation application". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 1 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Egrifta Prices, Coupons and Patient Assistance Programs". drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 1 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tesamorelin kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.