That Summer
"That Summer" ni wimbo uliotolewa na msanii wa miondoko ya Country wa Marekani Garth Brooks. Wimbo huu ulianzia katika albamu yake ya nne ya studio The Chase na pia ukaangaziwa katika on The Hits, The Limited Series na Double Live. Ilifika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Country za 1993. Wimbo huu ulitungwa na Garth Brooks, Pat Alger na Sandy Mahl.
“That Summer” | ||
---|---|---|
Single ya Garth Brooks | ||
B-side | "Dixie Chicken" | |
Imetolewa | Aprili 1993[1] | |
Urefu | 4:47 | |
Mtunzi | Pat Alger Sandy Mahl-Brooks Garth Brooks |
Hadithi ya Wimbo
haririWimbo unahusu mvulana mdogo ambaye huenda kumfanyia kazi mjane aliyetengwa ambaye alikuwa katika umbali wa maili ambayo ingefikika na kijana huyo. Usiku mmoja anamjia kijana huyo akivalia rinda ambalo hakuwa amevalia kwa muda mrefu. Pengine anarejelea rinda la ‘’kuchokoza hisia’’ na kuwa ni yeye peke yake aliyemwona kwa rinda hilo kwa muda sasa. Pia anagundua tofauti katika mtazamo wa mwanamke huyo. Wawili hao wanafanya mapenzi na wimbo unaendelea kwa kusema kuwa kila mara kijana huyo apitapo karibu na shamba la ngano anakumbuka msimu huo wa joto (summer) ambao walikuwa pamoja.
Garth Brooks aliongelea kuhusu utunzi wa "That Summer" katika kipindi maalumu cha televisheni cha "The Garth Brooks Story":
"That Summer ilianzia mwanaume kapera na mwanamke aliyeolewa wakikutana katika sherehe. Mwanamke huyo akipuuzwa kwa yule aliyekuwa naye, wanaenda na huyo kapera. Allen Reynolds anasema, “Sidhani ninapendezwa na watu aina hii.” Nilianza kufikiria pengine alikuwa na hoja. Nikienda nyumbani usiku huo katika lori nilianza kuimba, anahitaji kuhisi mngurumo (she has a need to feel the thunder). Sandy alinisaidia kuandika pambio na punde ikakamilika. Bila shaka jambo moja lakunifurahisha kuhusu That Summer ni kuwa inagusa hisia za kimapenzi."[2]
Mpangilio wa Vibao
haririEP Single ya Netherlands
hariri- "That Summer"
- "Shameless"
- "Friends in Low Places"
Nafasi katika Chati
haririChart (1993) | Kilele |
---|---|
U.S. Billboard Hot Country Singles & Tracks | 1 |
Canadian RPM Country Tracks | 1 |
Alitanguliwa na "Blame It On Your Heart" ya Patty Loveless |
Billboard Single ya kwanza 3 Julai 1993 |
Akafuatiwa na "Money in the Bank" wa John Anderson |
Alitanguliwa na "Hometown Honeymoon" ya Alabama |
RPM Country Tracks Singe ya Kwanza 10 Julai-17 Julai 1993 |
Akafuatiwa na ??? |
Virejeleo
hariri- ↑ Garth Brooks singles at LP Discography.com link
- ↑ "Transcription from "The Garth Brooks Story" (1996)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-14. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
Viungo vya nje
hariri- "That Summer" Lyrics Ilihifadhiwa 29 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.