The Austin Chronicle

The Austin Chronicle ni gazeti badala linalochapishwa kila wiki hasa katika siku ya Alhamisi. Mtindo wake wa uchapishaji ni ule wa gazeti la porojo na huchapishwa Austin,Texas Marekani. Gazeti hili husambazwa katika maduka ya magazeti yanayopatikana karibu na barabara, katika hoteli na katika mikahawa ambayo wasomaji wanaolengwa huzuru. Gazeti liliripoti kuwa lina wasomaji takriban 230,000.

The Austin Chronicle
Jina la gazeti The Austin Chronicle
Aina ya gazeti Gazeti badala la kila wiki
Lilianzishwa 1981
Eneo la kuchapishwa Austin,Texas
Nchi Marekani Marekani
Mhariri Louis Black
Mmiliki Shirika la Austin Chronicle
Mchapishaji Nick Barbaro
Makao Makuu ya kampuni 000 N I H 35
Austin, Texas 78751
Nakala zinazosambazwa 89,834
Machapisho husika *.Chronic
*. The Score
Tovuti www.austinchronicle.com
Ofisi kuu ya The Austin Chronicle.

Gazeti la The Chronicle lilianzishwa katika mwaka wa 1981 na mchapishaji Nick Barbaro na mhariri Louis Black, wakipata usaidizi kutoka kwa wenzao waliopatana katika programu ya Chuo Kikuu cha Texas ya masomo ya filamu. Barbaro na Black ,pia, ni waanzilishi wa Tamasha la South by Southwest ingawa tamasha hili huendeshwa na kampuni ingine tofauti.

The Chronicle huhusisha ,mara kwa mara, makala ya maoni na vipengele kuhusu vyakula, sinema,sanaa na muziki. Jarida hili huwa na makala mengine maalum ya kila mwaka kama tuzo za "Best of Austin", toleo la Halloween, toleo la Aprili Fool's na shindano la hadithi fupi. The Chronicle huwa ni mdhamini wa Tamasha la Austin Chronicle Hot Sauce, linaloandaliwa katika mwisho wa Agosti na hujulikana kwa kuwa na malengo ya kulinda mazingira.

Katika mwaka wa 2006, the Chronicle lilianzisha makala mawili katika tovuti yao yaliyoandikwa na waandishi wao: Chronic,linahusisha mitaa,jimbo,habari za kitaifa na habari za kisiasa; na The Score ,hili linaripoti kuhusu habari za michezo na halipatikani katika toleo la karatasi.

Wakosoaji wa filamu , Marjorie Baumgarten na Marc Savlov, ni waandishi wa makala ya The Chronicle na ,vilevile, ni wanachama wa Muungano wa wakosoaji wa Austin Film Critics.

Marejeo

hariri
  1. "Austin Chronicle". Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. Association of Alternative Newsweeklies.
  2. "Texas Music Industry Directory". Ilihifadhiwa 6 Januari 2009 kwenye Wayback Machine. Texas Music Office. 2001. pp. 23.

Viungo vya nje

hariri