The Book of Mormon (tamthilia ya muziki)

The Book of Mormon ni tamthilia ya muziki ya Marekani kutoka mwaka 2011. Iliandikwa na Trey Parker, Robert Lopez, na Matt Stone. Wao waliandika filamu ya South Park pia. The Book of Mormon ni tashtiti, na ilishinda tuzo nyingi[1].

Msuko wa tamithilia hariri

Tendo la kwanza hariri

Tamthilia inapoanza, Elder Price na wamormoni wengine wanaimba kuhusu kuzungumza na watu ambao hawaamini kanisa ya Mormoni. Wanapiga hodi nyumba za watu wengi, na wao hawataki kuzungumza kwa kawaida. Tunakutana Mormoni mwingine anayeitwa Elder Cunningham. Elder Price ni Mormoni nzuri sana, na wote wanafikiri kwamba yeye ni Mormoni bora kabisa. Elder Cunningham ni mtu mzuri, lakini hajui vitu vingi kuhusu kitabu cha Mormoni. Kila Mormoni anahitaji kwenda mji tofauti kwa miaka miwili anapokuwa na miaka kumi na nane, na Elder Price anataka kwenda mji wa Orlando. Kila mmisionari ana mbia mmoja ili wanaweza kusafiri pamoja, na kila Mormoni anataka kusafiri na Elder Price kwa sababu yeye ni Mormoni bora kabisa. Elder Price hataki kusafiri na Elder Cunningham, lakini wao wanahitaji kuwa timu pamoja. Mormoni mkuu anawaambia kwamba wanasafiri nchi ya Uganda kwa kufundisha kuhusu kitabu cha Mormoni.

Wanapofika nchi ya Uganda, wanajeshi wawili wanawaibia Elder Price na Elder Cunningham. Kingozi wa kijiji anawaambia kwamba mwanajeshi mkuu ni mbaya sana, na wanakijiji wanamwogopa sana. Pia, watu wanaoishi kijiji hawaamini Mungu. Baada ye kukutana Kiongozi wa kijiji, Elder Price na Elder Cunningham wanaona binti wa kiongozi. Yeye anaitwa Nabulungi, na Elder Cunningham anampenda sana kwa sababu Nabulungi ni mrembo.

Wanapofika nyumba mpya yao, Elder Cunningham na Elder Price wanakutana wamisionari wengine. Wana huzuni kwa sababu hakuna mtu mmoja anayetaka kuwa Mormoni. Elder Price anafikiri kwamba angeweza kubadilisha wanakijiji, lakini baada ya kuwahadithia historia ya Wamormoni, bado hawataki kuwa Mormoni. Mwanajeshi mkuu anasikiliza hadithi ya Elder Price, na anatisha wanakijiji. Mwanajeshi mkuu anaamini kwamba wanawake wanapaswa kuwa na tohara kwa wanawake (FGM). Kiongozi cha kijiji anawaambia kila mwanakijiji kwamba wanahitaji kukaa ndani ya nyumbani kwake, lakini Nabulungi anatake kuondoka na kujifunza kuhusa kitabu cha Mormoni. Elder Price kuna huzuni nyingi, na yeye anataka kurudi Marekani ili anaweza kusafiri mji wa Orlando kwa kufanya kazi ya mmisionari pale. Elder Cunningham anamwambia Elder Price kwamba atamfuata, lakini Elder Price anataka kusafiri pekee yake.

Tendo la pili hariri

Nusu ya pili ya tamthilia inapoanza, Elder Cunnigham anajaribu kufundisha wanakijiji kuhusu kitabu cha Mormoni bila Elder Price, lakini wanakijiji hawataki kusikiliza. Wanapoondoka, Elder Cunningham anaanza kudanganya kuhusu hadithi ya Mormoni. Anachanganya hadithi ya Mormoni na haditi za riwaya ya kisayansi kama The Hobbit na Star Wars.

Elder Price anaota jinamizi kuhusu mji wa Orlando kwa sababu anataka kuondoka nchi ya Uganda, na anapoamka, anakata shauri kurudi kijijini. Elder Cunningham anawathibitishia wanakijiji kubadili Mormoni, na anawabatiza. Elder Price ana wivu, lakini Rais wa wamisionari anakuja kijiji kwa kuona Wamormoni wapya. Wanakijiji wanahadithia Rais kuhusu vitu ambavyo wamefundishwa na Elder Cunningham, lakini si hadithi ya kitabu cha Mormoni kwa sababu Elder Cunningham alidanganya. Rais ana hasira sana na anawaambia Elder Cunningham na Elder Price kurudi Marekani. Kabla ya wanarudi Marekani, Nabulungi anamwambia Elder Cunningham kwamba wanakijiji walijua kila hadithi haikuwa kweli kabisa na kwamba zilikuwa na sitiari. Elder Cunningham na Elder Price wanarudi Marekani, lakini Wanakijiji wanaimba kuhusu kitabu cha Mormoni baada ya wao kuondoka.

Tanbihi hariri