The Kindness of Strangers (Heroes)
"The Kindness of Strangers" ni sehemu ya nne ya msimu wa pili wa tamthilia ya ubunifu wa kisayansi inayorushwa hewani na TV ya NBC - Heroes. Ilianza kurushwa hewani kwa mara ya kwanza mnamo tar. Oktoba 15, 2007. Kipengele hiki kinamtambulisha Monica Dawson kwa mara ya kwanza. Uhusika ambao ulichezwa na Dana Davis, ambaye alijiunga kama mshiriki mkuu.
"The Kindness of Strangers" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Maya and Alejandro find Sylar. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 2 Sehemu 4 | ||||||
Imetungwa na | Tim Kring | ||||||
Imeongozwa na | Adam Kane | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 15 Oktoba 2007 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
Hadithi
haririNathan Petrelli anatembelea watoto zake shuleni kwao. Anawaambia ya kwamba bibi yao (Angela Petrelli) amelazwa hospitali. Alipomtembelea mama'ke akiwa na Matt Parkman, amekiri ya kwamba yeye ndiye aliyehusika na kumsukuma Kaito Nakamura nje ya ghorofa. Matt, hata hivyo, anasoma mawazo yake na kumshauri Nathan ya kwamba alichokiri ni cha uwongo.
Anamwonesha Nathan picha ya Angela na Kaito iliyochorwa kwa mstari mwekundu na Nathan anampa Matt picha yenye orodha kamili ya watu waliohusika na kina Company. Picha ina-mwonesha Daniel Linderman, akiwa na wazazi wote wa Nathan (Angela na Arthur),[1] Bosi wa Mohinder Suresh Bob, Charles Deveaux, Kaito Nakamura, na watu wawili wasiojulikana, wanawake watatu wasiojulikana na mwanaume mmoja ambaye Matt alimtambua kama baba'ke, Maury.
Marejeo
hariri- ↑ Name revealed on 9th Wonders website Ilihifadhiwa 18 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya Nje
hariri- The Kindness of Strangers (Heroes) katika Internet Movie Database
- Beaming Beeman - Season 2, Episode 4 - Director's blog on the filming of this episode.