Theodora wa Turo

Theodora wa Turo (pia: Theodosia; Turo, Foinike, leo nchini Lebanoni, 290 hivi - Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 2 Aprili 307) alikuwa msichana Mkristo ambaye katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1] alijitokea hadharani kupongeza waliokuwa hukumuni kwa sababu ya imani yao[2]. Hivyo yeye pia aliteswa akakatwa kichwa[3][4].

Picha takatifu ya Mt. Theodora.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira mfiadini.

Sikukuu yake huadimishwa tarehe 2 Aprili[5][6].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.