Theodoro wa Studion

(Elekezwa kutoka Theodore of Studion)

Theodoro wa Studion (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 759[1] – Cape Akritas, Bitinia, 826) alikuwa mmonaki, halafu abati wa monasteri ya Studion mjini .[2]

Mt. Theodoro wa Studion katika mozaiki ya karne ya 11, Chios.

Alishika nafasi muhimu katika kufufua umonaki na fasihi huko Bizanti.

Kati ya vitabu vyake vingi, barua kuhusu urekebisho wa monasteri ndiyo maandishi ya kwanza kupinga utumwa.[3][4]

Anakumbukwa pia kwa kutetea kwa nguvu picha takatifu, bila kujali kwamba msimamo wake ulimvutia dhuluma kutoka kwa kaisari na patriarki zilizoathiri sana afya yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[5] au 12 Novemba.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Chisholm 1911, "Theodorus—Theodosia", p. 769.
  2. Browne 1933, p. 76; Chisholm 1911, "Theodorus—Theodosia", p. 769.
  3. Halsall, Paul (March 1996). Medieval Sourcebook: Theodore of Studium: Reform Rules. Fordham University. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-08-14. Iliwekwa mnamo 17 September 2012.
  4. Page 1929, p. 63.
  5. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.