Theodori wa Canterbury

(Elekezwa kutoka Theodoro wa Tarso)

Theodori wa Canterbury (Tarso, Kilikia, leo nchini Uturuki, 602 - Canterbury, Kent, Uingereza, 19 Septemba 690) alikuwa askofu wa mji huo kwa miaka 22.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha hariri

Msomi tayari, baada ya Waarabu kuteka mji wake (637) alihamia Konstantinopoli kuendelea na masomo mbalimbali, halafu mwaka 660 alihamia Roma katika monasteri ya Ukristo wa mashariki.

Papa Vitalian alimteua kuwa askofu mkuu wa Canterbury, akamweka wakfu tarehe 26 Machi 668.

Alirekebisha Kanisa la Uingereza lifuate mapokeo ya Roma akaanzisha shule ya Canterbury pamoja na Adriani wa Canterbury.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.