Tofu (豆腐, wakati mwingine pia doufu) ni chakula kilichotengenezwa kutoka kwa magandi ya maharagwe ya soya.

Kipande cha tofu ya Kijapani ( Kinugoshi tōfu )

Tofu hutengenezwa kwa kugandisha maziwa ya soya, na kisha kushinikiza magandi yanavyotokea kuwa imara zaidi. [1] Utengenezaji wa tofu kutoka kwa maziwa ya soya unafanana na mbinu ya kutengeneza jibini kutoka kwa maziwa ya ng'ombe au kondoo.

Huko China, Korea, Japani, Vietnam na Uthai tofu ni kati ya vyakula vya kawaida pamoja na wali.

Tofu ni hasa protini kwa hiyo inaweza kutoshekeza mahitaji ya mwili ya protini, sawa na nyama au samaki. Imekuwa moja ya misingi ya upishi wa ulaji mboga (vegetarian).

Tofu huwa la ladha hafifu tu, kwa hiyo inaweza kupikwa pamoja na vyakula vya kila aina ama vya chumvi au vitamu.

Katika nchi za Asia tofu hutumiwa kwa namna nyingi, ama bichi, au kupikwa, au kukaangwa, au kama sehemu ya supu au pamoja na mboga mbalimbali.


Vidokezo hariri

 

  1. "Japanese Tofu". www.japan-guide.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-05.