Tolnaftati
Tolnaftati, yaani Tolnaftate, inayouzwa chini ya majina ya chapa mbalimbali, ni dawa inayotumika kutibu magonjwa ya fangasi ikiwa ni pamoja na kuwashwa kutokanako na maambuki ya fangasi kwenye ngozi ya sehemu za siri, mapaja ya ndani na matako, mguu wa mwanariadha, muwasho utokanao na maambukizi ya fangasi inayosababisha muundo wa umbo la mduara kwenye ngozi, na maambukizi ya kawaida ya fangasi yanayosababisha mabaka madogo yaliyobadilika rangi kwenye ngozi (pityriasis versicolor).[1] Dawa hii iinatumika kwa ngozi.[1] Inapatikana kwa namna ya krimu, poda, vioevu vya kunyunyizwa na dawa iliyoyeyushwa.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mwasho wa ngozi.[1] Ni katika kundi la kabameti ambazo zina sulfuri (thiocarbamate).[1]
Tolnaftati ilitengenezwa karibu mwaka wa 1962.[2] Inapatikana kama dawa ya kawaida na kuuzwa kwenye kaunta.[1][3] Nchini Marekani, mrija wa gramu 28 wa dawa hii inagharimu takriban dola 6 kufikia 2021.[3] Inapatikana pia nchini Uingereza bila agizo la daktari.[4]
Marejeleo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Tolnaftate Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Greenwood, David (21 Februari 2008). Antimicrobial Drugs: Chronicle of a Twentieth Century Medical Triumph (kwa Kiingereza). OUP Oxford. uk. 360. ISBN 978-0-19-953484-5. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2021.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 "Compare Tolnaftate Prices - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 1294. ISBN 978-0-85711-369-6.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)