Trofinetide, inayouzwa kwa jina la chapa Daybue, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa Rett (hali ya neva ya kurithi inayathiri hasa wasichana na inajulikana kwa kushindwa katika maendeleo ya akili na ya kimwili).[1] Dawa hii inatumika kwa watu angalau miaka miwili [1] na inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara na kutapika.[1] Kupoteza uzito kunaweza kutokea pia.[1] Matumizi yake hayapendekezwi kwa wale walio na matatizo makubwa ya figo.[1] Jinsi inavyofanya kazi haijulikani.[1]

Trofinetide iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2023.[1] Kwa wale walio na uzito wa chini ya kilo 12 itagharimu takriban dola 385,000 za Marekani kwa mwaka, wakati kwa wale ambao ni zaidi ya kilo 50 itagharimu takriban dola 924,000 za Marekani kwa mwaka nchini Marekani kufikia mwaka wa 2023.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "DailyMed - DAYBUE- trofinetide solution". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Julai 2023. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"DailyMed - DAYBUE- trofinetide solution". dailymed.nlm.nih.gov. Archived from the original on 2 July 2023. Retrieved 12 June 2023.
  2. "FDA Approves First Treatment for Rett syndrome". Formulary Watch (kwa Kiingereza). 13 Machi 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Mei 2023. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Trofinetide kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.