Tume ya Uchaguzi ya Kenya

Tume ya Uchaguzi ya Kenya sasa inarejelea tume ambayo ilibatiliwa na bunge ya kumi mwaka wa 2008 na ilipokelewa na tume ya 'Interim Independent Electoral Commission of Kenya'. Samuel Kivuitu ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume hiyo ilipobatiliwa, alienda kortini Novemba 2008 kupinga uamuzi huo.[1] Walidai kuwa uamuzi huo haukuambatana na katiba kwani tume ilifaa kuwekwa ili kuchunguza makosa waliodaiwa kuyafanya katika uchaguzi mkuu wa 2007. Kesi hiyo itaendelea 3 Februari 2010 katika korti ya katiba.[2]

Tazama Pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. [0] ^ "Court halts bid to disband ECK" Daily Nation, Novemba, 11, 2008
  2. "ECK commissioners’ suit to be heard in February" Archived 16 Julai 2011 at the Wayback Machine. The Standard, 17 Novemba 2009