Tunguhina
Tunguhina kaskazi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Jenasi: Uraeginthus (Tunguhina na vitenduli)
Cabanis, 1851
Ngazi za chini

Spishi 2:

Tunguhina ni ndege wadogo wa jenasi Uraeginthus katika familia ya Estrildidae ambao wana rangi kahawianyekundu na viraka buluu au zambarau. Kuna spishi tatu zingine kwa jenasi hii ambazo zinaitwa vitenduli na zina rangi buluu. Wataalamu wengine wanaweka spishi mbili za tunguhina ndani ya jenasi Granatina. Spishi hizi zinatokea Afrika chini ya Sahara tu. Tunguhina ni ndege waoga, lakini kwa bustani ya hoteli na nyumba wanazoea watu. Tago lao hutengenezwa na manyasi ndani ya magugu; limefunikika juu na lina mwingilio kando.

Spishi hariri

Picha hariri