Tuzo za Zim Hip Hop

Tuzo za zim hip hop,pia inajulikana kama Tuzo za Hip Hop za Zimbabwe (kwa kifupi kama ZHHA) ni tukio la kila mwaka la tuzo linaloundwa ili kuwatambua wasanii bora wa hip hop wa Zimbabwe nchini Zimbabwe pamoja na wasanii wa hip hop wanaoishi ughaibuni. Tuzo hizo hutolewa Desemba kila mwaka.[1]

Historia hariri

Tuzo za Hip Hop za Zimbabwe zilianzishwa Desemba 2011 na toleo la kwanza lilifanyika katika ukumbi wa (7 Arts Theatre) huko Harare na kuwa sherehe ya kwanza ya tuzo kwa wasanii wa hip hop nchini Zimbabwe. Tuzo hizo zimekuwa muhimu katika kuweka hip hop ya Zimbabwe kwenye ramani ya kitaifa na kikanda.[2]

Marejeo hariri