Ubaridi ni uwepo wa hali ya chini ya halijoto katika kitu fulani au eneo fulani, lakini hasa katika angahewa. Katika hali ya kawaida baridi huwa ni hali ya mtazamo binafsi. Mpaka wa chini kabisa wa baridi ni sifuri halisi ambayo katika skeli ya Kelvin husomwa kama 0.00K.

Siwa barafu ambalo kwa kawaida husababishwa na baridi.

Kwa kuwa halijoto huhusisha nishatijoto inayoshikiliwa na kitu au sampuli ya maada, ambayo ndiyo nishati mwendo ya chembe ziundazo maada, kitu kitakuwa na nishatijoto ndogo pale kinapokuwa cha baridi na nishatijoto kubwa pale kinapokuwa cha moto.

Kama kungalikuwa na uwezekano wa kuupooza mfumo fulani mpaka halijoto ya sifuri halisi, mwendo wote wa chembe katika sampuli ya maada ungekoma and chembe hizo zingekuwa tuli katika mtazamo huu wa kisasa. Kitu hicho kingechukuliwa kuwa na nishatijoto ya sifuri.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubaridi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.