Uchaguzi Mkuu wa Malawi, 2004


Uchaguzi wa Urais na Bunge ukifanyika nchini Malawi mnamo 20 Mei 2004. Uchaguzi huu ulikuwa umepangiwa kutendeka mnamo 18 Mei lakini ukahairishwa kwa siku mbili kufuatia mwitikio kwa madai ya wapinzani kuhusu udanganyifu katika sajala ya wapiga kura.[1].

Malawi

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Malawi



Nchi zingine · Atlasi

Kufikia 22 Mei, hakuna matokeo yalikuwa yametangazwa, jambo lililoonekana kutishia amani. Mnamo 25 Mei, Tume ya Uchaguzi ya Malawi hatimaye ilitangaza matokeo. Bingu wa Mutharika, mgombezi wa urais kwa chama cha United Democratic Front, alitangazwa kuchaguliwa. Mutharika alikuwa akiungwamkono na rais anayeondoka Bakili Muluzi, ambaye alisaafu baada ya kuhudumu kwa vipindi viwili. Malawi haina Kura za maoni za kutegemewa lakini utafiti uliofanywa na vyombo vyya habari vya Malawi kabla ya uchaguzi ulikuwa umemweka Gwanda Chakuamba, mgombea wa mrengo wa vyama saba kuwa aliyepigiwa upato kuongoza.

Jedwali la Matokeo hariri

Mgombea Chama Kura %
Bingu wa Mutharika United Democratic Front 1,119,738 35.9
John Tembo Malawi Congress Party 846,457 27.1
Gwanda Chakuamba Mgwirizano Coalition 802,386 25.7
Brown Mpinganjira National Democratic Alliance 272,172 8.7
Justin Malewezi People's Progressive Movement 78,892 2.5
Invalid/blank votes 86,218 -
Jumla 3,205,863 100
Chanzo: EISA

Wagombea Urais hariri

  • Bingu wa Mutharika, mkongwe wa miaka sabini na mwanauchumi, alikuwa mgombea kwa tiketi ya CHama cha United Democratic Front, ingawa awali alikuwa mpinzani wa chama hicho. Aliungwa mkono na rais anayeondoka, Muluzi.
  • Gwanda Chakuamba, mwenye umri wa miaka 69, alikuwa akigombea kwa tiketi ya Muungano wa Mgwirizano au Muungano wa Umoja ambao ulishirikisha vyama saba. Chamwamba aliwahi kuwa waziri wa ngazi ya juu na komanda wa jeshi la militia. Mnamo 1980 alizozana na Banda, na akashtakiwa kupanga mauaji yake. Alikaa miaka 12 gerezani na hili likamfanya shujaa maarufu na hatimaye akamrithi Mpanda katika nafasi yake ya uongozi wa Chama chake cha Malawi Congress Party.
  • John Tembo, wa umri wa miaka 72, alikuwa mgombea kutoka chama cha Malawi Congress.

Uchaguzi wa Bunge hariri

Bunge la Malawi lina wabunge 192. Kulingana na BBC, Chama cha Malawi Congress kilishinda viti ‘’’60’’’, United Democratic Front kikashinda 49, Muungano wa Mgwirizano ukazoa viti 28 na wagombea wa kibinafsi wakanyakua viti 38. Katika Uchaguzi Mkuu wa Malawi wa 1999, United Democratic Front ilikuwa imeshinda viti 93, Malawi Congress Party kikashinda viti 66, huku Alliance for Democracykikishinda viti 29.

Wakaguzi wa Kimataifa hariri

Tasisi ya Uchaguzi ya Afrika Kusini ilituma wakaguzi nchini Malawi kwa uchaguzi wa urais na bunge wa 2004[2].

Marejeo hariri

  1. "Special report on general elections", IRIN, 19 Mei 2004.
  2. Ott, Martin. The power of the vote: Malawi's 2004 parliamentary and presidential elections. Kachere Series, 2005. p. 296. ISBN 9789990876581.  Found at Google Books

Viungo vya nje hariri