Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1876

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1876 ulikuwa wa 23 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 7 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rutherford Hayes (pamoja na kaimu wake William Wheeler) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Samuel Tilden (pamoja na kaimu wake Thomas Hendricks).

Matokeo hariri

Hayes akapata kura 185, na Tilden 184. Kura 20 za Hayes zilikuwa zimeafikiana kati ya vyama vigombea, na matokeo yanaendelea kujadiliwa na wataalamu wa historia. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.